MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemuomba Rais John Magufuli kutafakari upya kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (Pichani) bado anafaa kuongoza Wizara hiyo, kufuatia wimbi la matukio yanayoashiria ukosefu wa usalama nchini.
Lema, ambaye ni waziri kivuli wa wizara hiyo, alisema hayo jana, wakati akizungumzia kauli za Mwigulu aliyoitoa juzi kuhusu kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na matukio mengine, yakiwamo ya kupotea kwa aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Ben Saanane.
“Jana (juzi) nilifikiria Mwigulu angeachana na ngonjera zake akaongelea habari angalau ya maslahi ya askari hawa, Mwigulu amenisikitisha sana, na sidhani kama anastahili kukaa kwenye ile ofisi hata kwa saa mbili.
“Yeye kama Waziri wa Mambo ya Ndani, tangu Lissu ameshambuliwa hajawahi kurusha hata mguu Nairobi, hata kwenda kuongea na Waziri wa Mambo ya Ndani Kenya, kuomba ulinzi kwa ajili ya mgonjwa.
“Wakati ni mbunge mwenzake, tena wa mkoa wake amepigwa risasi, ila hajishulishi, jana anaongea vitu vyepesi kuhusu maisha ya watu, kwa kauli zake kama
kuna mtu alimtazama wakati anaongea, utajua tukio la Lissu limefanywa na nani, na nani yuko nyuma ya tukio hili, vinginevyo angekuwa na ujasiri wa kuelekeza polisi kutafuta wahalifu kwa nguvu zote, angewaza pengeni anayefuata ni yeye,” aliongeza.
“Serikali ijue tu kama tukio hili la Lissu haliko connected na wao, waliofanya tukio hili wana nia mbaya,” alisema Lema.
BEN SAANANE
Kuhusu kauli ya Mwigulu kuwa hawezi kusema alipo Saanane, ni dhairi kuwa polisi haitaweza kufanya uchunguzi wa tukio la Lissu.
“Waziri anaongea kirahisi sana kama anaongea kwenye birthday, kirahisi sana, hicho anachokifanya baadaye Rais atajua walikuwa hawamsaidii na mimi nina uhakika siku zake katika ofisi ya Wizara hiyo zinahesabika.”
KUJENGA NYUMBA ZA POLISI
Katika hatua nyingine, Lema amemuomba Rais Magufuli kuchukua hatua za kuhakikisha serikali inajenga nyumba za kisasa za Polisi waliounguliwa nyumba zao hivi karibuni mkoani Arusha, kama alivyochukua hatua za kujenga ukuta kuzunguka eneo la migodi ya tanzanite Mererani.
Lema alidai Polisi mkoani hapa wanaishi kwenye nyumba mbovu na mbaya, ikizingatiwa kazi yao ni kulinda usalama na maisha ya watu na mali zao.
Alisema kuwa, tukio la kuunguliwa nyumba askari hao linapaswa kuchukuliwa hatua za haraka, kwa kuwa linagusa maisha ya watu na familia zao.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ GODLESS LEMA AMCHONGEA MWIGULE NCHEMBA KWA RAIS JOHN MAGUFULI KISA TUNDU LISSU, BEN SAANANE
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment