MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI APATA AJALI, BABA YAKE MZAZI AFARIKI DUNIA PAPO HAPO
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Pwani (SSP) Abdi Issango amelazwa kwenye Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha Mkoani Pwani baada ya kupata ajali.
Kamanda huyo amepata ajali Septemba 16, saa kumi jioni Kijiji cha Kibiki Wilaya ya kipolisi ya Chalinze mkoani humo akiwa na familia yake ambapo baba yake mzazi alifariki papohapo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Jonathan Shanna amemtaja marehemu kwamba anaitwa Hamis Issango, huku akisema mama yake mzazi alijeruhiwa vibaya huku ndugu yake mmoja akipoteza maisha.
"Ajali imesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi wanne akiwemo Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani na aliyefariki ni baba yake’’alisema
Pia amesema majeruhi wengine ni mdogo wake ambaye ni mwanafunzi hao wote wamelazwa kwenye Hospital ya Tumbi.
Amesema kamanda huyo alikuwa akisafiri na familia yake hiyo kutokea Singida kuelekea Kibaha na waliligonga kwa nyuma lori lillokuwa limeharibika barabarani.
Kamanda shanna amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa lori aliyeshindwa kuweka alama za kuashiria gari lake ni bovu alilokuwa ameliegesha pembezoni mwa barabara.
Kamanda Shanna amesema dereva wa lori hilo na utingo wake walikimbia, polisi wanaendelea kuwatafuta.
0 comments:
Post a Comment