BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAHCO YABOMOA NYUMBA 21 NA KUWAACHA ZAIDI YA WAKAZI 80 WAKIKOSA MAKAZI MORO

Mkazi wa mtaa wa Mkwajuni kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro, Maua Juma akiwa na mtoto wake pembeni ya mabaki ya nyumba yake baada ya zaidi ya watu 80 kutoka kaya 21 kukosa sehemu ya kulala kufuatia nyumba za kubomolewa na kampuni hodhi ya rasimali za reli nchini (RAHCO) kwa madai ya kujenga ndani ya eneo la shirika hilo tangu septemba 9 mwaka huu. Picha na Juma Mtanda.

Juma Mtanda, Morogoro.
Zaidi ya wakazi 80 kutoka kwenye kaya 21 wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wamekosa sehemu ya kulala baada ya nyumba za wazazi wao kubomolewa na kampuni hodhi ya rasimali za reli nchini (RAHCO) eneo la mtaa Mkwajuni kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro.

RAHCO imeendelea zoezi la kubomoa nyumba zinazodaiwa kujengwa ndani ya hifadhi ya reli ya kati baada ya baraza la ardhi la wilaya ya Morogoro kutoa hukumu ya pingamizi lililowekwa na baadhi ya wakazi wa mtaa huo kupinga kubomolewa nyumba zao.

Wakizungumza na MTANDA BLOG eneo la tukio mjini hapa, walisema kuwa kitendo kilifanywa na uongozi wa reli ni cha uonevu na mpaka sasa zaidi ya watu 80 kutoka kwenye kaya 21 hawana makazi ya kuishi na kulazimika kulala nje katika mazingira magumu baada ya nyumba zao kubolewa bila kufuata taratibu za kisheria tangu Septemba 9 mwaka huu.

Katibu wa wahanga hao, Aminatha Rashid Msusa amesema kuwa nyumba 21 ndio zilizokumbwa na bomoaboa hiyo na kusababisha wakazi zaidi ya 80 kukosa sehemu ya makazi wakiwemo watoto 42, wanafunzi 31 wa sekondari na msingi ambao kwa sasa wanalala nje kando ya nyumba zao zilizobomolewa.

Aminatha alieleza kuwa katika bomoabomoa hiyo sehemu kubwa ya vyakula vilivyokuwa ndani ya nyumba zao vimeharibiwa na kuzua hofu kutokana na miezi miwili iliyopita ilikuwa msimu wa mavuno kutokana na kuwa na muda mdogo wa kuokoa mali na vyakula.

“Tunagombea mipaka kati ya reli na mtaa wa Kikwajuni katika kata hii ya Kichangani na tumepinga sisi kuondolewa na kesi ipo mahakamani na kesi yake imepangwa kusikilizwa Septema 25 mwaka huu lakini kabla ya kesi kusikilizwa tukio hili linatokea na inasikitisha sana.”alieleza Aminatha.

Aminatha alidai kuwa eneo hilo tangu mwaka 1974 watu wamekuwa wakiendesha maisha bila bughuza.

Afisa Mahusiano wa RAHCO, Catherine Mushi akiongea kwa njia ya simu na gazeti hili alieleza kuwa wamekuwa wakitoa taarifa kwa wananchi wote waliovamia maeneo ya reli na hifadhi zake kinyume na sheria, taratibu baada ya kuwekewa alama ya kuondoka kwa hiyari kufuatia maeneo hayo kuvamiwa.

Catherine alieleza kuwa watu wote waliobomolewa wamekuwa wakaidi baada ya uongozi kutoa tahadhari ya kuwataka wavamizi wote waliovamia kuhama kwa hiyari lakini baadhi yao wamekuwa wakibomoa nyumba zao kwa hiyari na wengine kukagaidi.

Mwanafunzi wa Maimuna Seleman shule ya msingi Mkwajuni kata ya Kichangani alieleza kuwa bomoamoboa hiyo imetoa siku ya mapumziko na kujikuta vifaa vya shule kuhabiliwa baada ya kufukiwa na kifusi.

Maimuna alieleza kutokana na vifaa vya shule kufukiwa na kifusi anaoma wasamalia wema kuweza kumsaidia vifaa vyote vya shule ikiwemo madaftari, mikebe, kalamu, penseli ili kuweza kuhudhiria vyema masomo.

Kwa upande wa, Mary Samuel alieleza kuwa bomoaboma hiyo imefanyika wakati akiwa msibani na aliporejea tayari nyumba yake ilikuwa inabomolewa na kushindwa kukoa baadhi ya mali kikiwemo chakula.

Mary alieleza kuwa kalandika limempotezea mwelekeo wa maisha yake ilhasi maisha yao yapo mashakani na wamekuwa wakitegemea chakula kutoka kwa majirani na hali itakuwa ngumu kwa upande wa wanafunzi wanaohitaji utulivu sehemu ya kulala ili kuhudhuria vyema shuleni.

“Baadhi ya viongozi wamekuwa kando nao na wanajihisi wakimbizi kutokana na kutengwa baada ya tukio kutokea kwa kushindwa kuwafariji ama kuwatolea ufafanuzi kwani walifungua kesi mahakama kupinga kubomolewa.”alieleza Mary.

Kutokana na kukosa mahali pa kwenda baadhi ya wakazi hao waliobomolewa makazi yao wameendelea kusalia katika maeneo hayo kwa kujenga vibanda vidogo vidogo kwa lengo la kujistili kwa muda.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: