BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BORIS YELTSIN, RAIS ‘CHAPOMBE’ ALIYETOROKA IKULU USIKU KWENDA KUTAFUTA CHAKULA



Na Geofrey Chambua
Hebu vuta picha, ni saa nane za usiku unakimbizana na muda kuwahi kurudi nyumbani baada ya kuchelewa kwenye mihangaiko yako, ukiwa unakatiza mitaa ya karibu na ikulu, unakutana na kitu kinachokufanya usiyaamini macho yako.



Unakutana uso kwa uso na mheshimiwa Rais, akiwa anayumbayumba kutokana na kuzidiwa na pombe, tena akiwa amevaa bukta ya kulalia tu, yuko bize kusimamisha teksi eti zimpeleke kwenye mgahawa ambao uko wazi akanunue msosi kwa sababu anasikia njaa kali. Utahisi upo ndotoni si ndiyo?

Basi kwa taarifa yako tukio kama hilo limewahi kumkumba aliyekuwa Rais wa Urusi, Boris Yeltsin. Wakati wa utawala wa Rais Bill Clinton wa Marekani, mwaka 1995 alimualika Yeltsin, akiwa rais wa Urusi wakati huo kwenda kumtembelea kwenye Ikulu ya White House jijini Washington.

Licha ya kwamba Yeltsin alikua kivutio kikubwa nchi za nje, lakini wengi Urusi kwenyewe watamkumbuka kwa kuwa chanzo cha kuanguka taratibu kwa taifa hilo kubwa.



Yeltsin alikua ni kiongozi aliyezusha mabishano wakati wote, akichomoza kama mwanasiasa wa enzi ya ukoministi aliyejitolea kupambana na rushwa, lakini akashindwa hatimae kuzuwia ubadhirifu wa mali , hasa wakati wa zoezi la ubinafsishaji wa viwanda vya dola.

Sambamba na hayo alikua rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasi na kuitawala Urusi kwa muda wa miaka tisa, kabla ya kumuachia madaraka rais wa sasa Vladimir Putin aliyemteuwa na kumpigia debe kuwa mrithi wake.

 
Miongoni mwa shutuma kali alizopambana nazo ni msimamo wake wa kuiingiza Urusi vitani dhidi ya waasi katika jimbo la Chechnya, waliokua wakipigania kujitenga jimbo hilo—vita ambavyo viliitia aibu Urusi na kulazimika kujiondoa.

Sifa kubwa ya Yeltsin, kabla hajawa rais, alipokuwa rais na mpaka alipostaafu, ilikuwa ni kupiga mitungi mpaka anakuwa chakari. Basi baada ya shughuli zote za kiofisi kukamilika ikulu, jamaa alianza kujimiminia Vodka kwa uchu mpaka akawa tilalila. Kibaya alikuwa anakunywa bila kugonga msosi.

Akapitiwa na usingizi lakini mishale ya saa nane za usiku, alizinduka, pombe zikiwa bado kichwani na kukumbuka kwamba hakula usiku huo zaidi ya kupiga maji. 


Kutokana na njaa iliyokuwa inamsumbua, akaona isiwe tabu, akatoka akiwa amevaa bukta na kuwazidi ujanja walinzi wa ikulu, akaingia mitaani na kuanza kupiga kelele kusimamisha teksi impeleke kununua pizza.


 Walinzi wa ikulu kuja kushtukia, rais tayari alishafika Mtaa wa Pennsylvania huku akiendelea kufanya mambo ya kilevi, wakagundua kuwa kumbe mtu huyo alikuwa rais wa Urusi, wakawa wanajiuliza imekuwaje awapite bila kumtambua?
Harakaharaka wakaenda kumchukua na kumrudisha ndani huku mlinzi mmoja akitumwa kwenda kumnunulia pizza kwani mwenyewe bado alikuwa akilalamikia njaa.

Kutokana na itifaki za White House, tukio hilo lilifanywa kuwa siri kubwa kuanzia siku linatokea mpaka miaka kumi baadaye, Rais Bill Clinton ndiye aliyeamua kulisimulia alipoamua kuandika kitabu cha kumbukumbu za maisha yake.

Kwa mara ya kwanza, Clinton alimsimulia mwandishi Taylor Branch aliyeandika kitabu cha historia ya Clinton kilichopewa jina la The Clinton Tapes: Wrestling History with the President. Rais Yeltsin alifariki miaka miwili iliyopita baada ya kuugua.

Mnamo mwaka 1996 John Major alimualika Boris Yeltsin Downing Street kwa mazungumzo ya kikazi. AKIWA Ameamua kuupiga nyingi tangu anaondoka kwake alifika London rais amelewa kuepusha aibu ndege iligeuza

Warusi wanakwambia walikua wanaona haya kuwa Rais wao 'Mzee yule ni cha pombe kiasi kwamba kipindi cha kampeni ya uraisi (1995) kuna sehemu walimuandalia kwa ajili ya malazi. 


Kumbe walikuwa wanamfahamu bwana, kamati ya maandalizi/mapokezi waliandaa gari zima (landrover za zamani) likiwa limejaa pombe. tulijiuliza kuna sherehe wapi siku hiyo (kama unavyojua mikoani kipindi hicho kila kinachoendelea kinafahamika kwa wakazi wote). 

Kuja kugundua zinaingizwa kwenye lodge ya mzee mzima, kesho yake aliondoka tukashuhudia yanatoka matupu tu. 

Kuna askari wa eneo hilo nao walipata nafasi ya kushirikiana na walizi wa mzee katika doria usiku huo, wakatudokeza kuwa mzee kakesha anakuywa, ilifikia wakati alianza kucheza mziki
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: