BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WILAYA YA MVEMERO MBIONI KUMALIZA UTATA NA MANUNG'UNIKO YA MIGOGORO YA ARDHI MOROGORO

Afisa ardhi mteule wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Keneth Mwenda akizungumza jambo wakati wa mkutano wa hadhara wa kutatua migogoro ya ardhi uliofanyika ofisi ya kijiji cha Wami Sokoine wilayani humo, wa Kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Kulwa Patrick na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Pakurisi Nakuroy. Picha na Juma Mtanda.

Juma Mtanda, Morogoro.
Halmashauri ya wilaya ya Mvomero ipo mbioni kumaliza utata na manung’uniko kutoka kwa wananchi 55 wa kijiji cha Wami Sokoine kata ya Dakawa baada ya nyuma zao 34 kufanyiwa tathimini na kushindwa kuwalipa kwa wakati, fidia ya fedha tangu mwaka 2006 walipoachia maeneo yao kuingia serikalini mkoani Morogoro.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika juzi ofisi ya kijiji cha Wami Sokoine mkoani hapa, walisema kuwa wamekuwa wakiishi maishi ya dhiki na tangu kwa miaka 11 kwa kulala kwenye nyumba zilizokosa ubora baada ya serikali kusitishwa shughuli za maendeleo ili kupisha maeneo yao kuingia katika mpango wa matumizi mbalimbali ya wilaya ya Mvomero.

Mkazi wa kitongoji cha kanisani, Emmanuel Shabala alisema kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mvomero aliandikiwa barua ya maombi mbalimali likiwemo la marekebisho ya tathimini ya viwanja vilivyopo usoni mwa wilaya katika kata ya Dakawa.

Shabala alisema kuwa moja ya ombi hilo ni bei ya mita za mraba sh2000 na kuomba walipwe fidia kwa bei iliyopo sokoni hivi sasa ya mita za mraba sh3000 pamoja na kutambua nyumba zote zilizofanyiwa tathmini tangu mwaka 2006 na hivi sasa kubomoka.

“Kuna nyumba 34 zimefanyiwa tathimini tangu mwaka 2006 lakini mwaka huu halmashauri imerudia tena kufanya tathimini na kutotambua nyumba zilizobokoa na tunaomba viwanja vilizopewa mabwenyenye na wameshindwa kuendeleza wanyang’anywe na kupewa wanaWami Sokoine.”alisema Shabala.

Katika fomu ya fidia, kumebainishwa kuwa na fedha ya kujikimu ya sh10,000 lakini tunaiomba halmashauri ilipe sh50,000 kwa mwezi, kwani sh10,000 kwa mwezi haikithi mahitaji kutokana na idadi ya familia na maisha ya sasa kuwa juu.alisema Shabala.

Mwenyekiti wa kijiji cha Wami Sokoine, Pakurisi Nakuroy alisema kuwa mkutano huo wa hadhara ulikuwa na ajenda mbalimbali za kutafuta ufumbuzi migogoro mbalimbali kati ya wananchi na afisa ardhi mteule wilaya ya Mvomero, Keneth Mwenda.

Nakuroy alitaja ajenda hizo kuwa ni watu wanaokaa mbele ya uso wa wilaya Mvomero kusimashwa kutojenga tangu miaka 2006, watu wanaokaa maeneo yaliyopimwa kinyume cha sheria, migogoro ya mipaka kati ya kijiji cha Luhindo na Wami Sokine na changamoto ya wananchi kukosa maeneo ya kulima na kufuga mifugo ya asili.

Natoa wito kwa wananchi wa Wami Sokoine kufanya subira kwani mambo yanaenda ukingoni na kila mtu atapata haki yake.alisema Nakuroy anayeongoza wakazi 2500 katika kijiji cha Wami Sokoine.

Kwa upande wa Afisa ardhi mteule wilaya ya Mvomero, Keneth Mwenda alisema kuwa halmashauri imejipanga kuondoa na kumaliza utata na manung’uniko juu ya ulipaji wa fidia na mpango huo sasa umeiva isipokuwa viongozi wawili wamebakia kutia saini fomu za kulipa fidia ili zoezi la ulipwaji ufanyike.

Mwenda alisema kuwa wananchi wa Wami Sokoine wanapaswa kuwa na subira kwani kipindi cha siku chache zijazo, Mkuu wa mkoa na wilaya Mvomero watakuwa wametia saini za nyaraka za fidia kwa watu 55 baada ya nyumba 34 kufanyiwa tathimini.

“Halmashauri ya Mvomero inajua kero hii imekaa muda mrefu lakini viongozi tuliopo hakuna aliyekaa kwa zaidi ya miaka miwili, hivyo tumefanya jitihada na tumefuatilia na sasa zoezi linaelekea ukingoni kwani nyaraka za malipo ya fidia zetu tunasuiri mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya watie saini ili kila mtu amepewe haki yake.”alisema Mwenda.

Mwenda alisema kuwa changamoto ya uhaba wa mashamba, maeneo ya malisho ya mifugo ya asili na changamoto nyingine zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Tayari halmashauri ya Mvomero ina hekali za ardhi 12,200 baada ya mashamba matatu kupokonywa wamiliki na hekali hizo zitagawiwa kwa utaratibu maalumu ili wakazi wa Wami Sokoine waweze kupewa.

Mwenda alisema kuwa halmashauri itawaondoa watu waliovamia kitalu J na kuishi na kinyume cha sheria lakini wavamizi hao wamepewa nafasi ya upendeleo kwa kupewa nafasi ya kuandika barua ya maomi ili kumilikishwa kihalali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: