TRENI YA ABIRIA ILIKUWA INAENDA KIGOMA YAPATA AJALI WILAYA YA UVINZA
Treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania iliyokuwa ikitokea mkoani Dodoma kwenda Kigoma imepata ajali katika eneo la Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza.
Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na kusababisha mabehewa mawili kuanguka katika dimbwi dogo la maji.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Othieno hadi sasa hakuna taarifa za kutokea kwa vifo wala idadi ya majeruhi.
Behewa kadhaa bado zimesalia kwenye njia yake baada ya ajali.
Kwa taarifa/AZAM TWO.
0 comments:
Post a Comment