BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HUZUNI IMETANDA SIKU 100 TANGU AZORY GWANDA ATOWEKE KATIKA MJI WA KIBITI PWANI KATIKA MAZINGIRA YA UTATA

Ni siku 100 tangu kutoweka kwa Mwandishi Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania aliyetoweka mwezi wa November mwaka jana.

Francis Nanai Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications, MCL, amesema wataisaida familia ya mwandishi huyo kwa kulipia ada za watoto, bima ya afya na mtaji biashara kwa mke wa Azory ili aweze kujikwamua kiuchumi.

Mpaka sasa MCL hawana ripoti yoyote toka chombo chochote cha ulinzi na usalama juu ya kupotea kwa Azory.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali na kampuni ya magazeti ya mwananchi, mwanahabari huyo wa kujitegemea alitoweka tarehe 21 Novemba.
 

Gwanda alikuwa anaishi na kuripoti kutoka mji mdogo uitwao Kibiti, ambao upo kilomita kama 130 hivi kusini mwa Dar es Salaam.

Bwana Gwanda ni mmoja wa waaandishi wa kwanza kabisa kuripoti kwa kina juu ya mfululizo wa mauwaji yaliyokuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana yaliyowalenga polisi na viongozi wa mji huo.

Mauwaji hayo yaliyotokea miezi kadhaa tu iliyopita yalitia hofu kubwa mjini hapo.
Siku ya 17 : Wafanyakazi wa kampuni ya Mwananchi walivalia mavazi meusi katika kikao na wanahabari.

Mke wake Anna Pinoni alisema watu wapatao wanne wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walimchukua bwana Gwanda kutoka katikati ya mji huo, mahali ambapo hupendelea kukaa.

Anasema pia aliporudi nyumbani alikuta vitu vimezagaa, ishara kwamba inawezekana waliipekua nyumba yao.

Azory aliwasiliana na ofisi za Mwananchi mara ya mwisho tarehe 20 Novemba kwa majukumu ya kikazi.
Visa vya mauaji ya kutoweka kwa watu Tanzania.


Mauaji ya Kibiti mwaka 2017: Viongozi wa CCM, askari zaidi ya 10 na wananchi karibu 40 katika eneo la Kibiti walishambuliwa na kuuawa na watu wasiojulikana.


11 Februari, 2018 Kiongozi wa Chadema Daniel John alitekwa na kisha aliuwawa kikatili wakati wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni. Mwili wake ulipatikana mnamo 14 Februari.


Mnamo 7 Septemba, 2017, Mnadhimu Mkuu wa upinzani bungeni, mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Area D Mkoani Dodoma. Bw Lissu pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika.


21 Novemba, 2017 Mwandishi wa habari wa Mwananchi Communications Limited Azory Gwanda alipotea katika mazingira ya kutatanisha na mpaka sasa hajapatikana.


Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Ben Saanane alipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: