POLISI WATANO WAPOTEZA MAISHA BAADA YA KUSHAMBULIWA KIKOMANDOO
Washambuliaji wa kwanza walipiga mnara wa Kampuni ya Simu ya Safaricom katika Mji wa Lafey, kwa lengo la kukata mawasiliano kati ya maofisa na mabosi wao, kabla ya kuvamia kambi hizo.
Maofisa watano wa polisi wameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa baada ya watu wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab kushambulia kambi mbili za usalama zilizoko Fino katika kaunti ya Mandera.
Naibu Kamishna wa wilaya ya Lafey, Eric Oronyi amesema shambulizi hilo lilifanywa saa 7:00 usiku na lililenga kambi ya maofisa wa polisi na utawala wa polisi katika mji wa Fino.
"Lilifanyika shambulizi katika makambi mawili ya usalama Fino na hivi tunavyozungumza, maofisa watano wamekufa na wengine watatu wamejeruhiwa," amesema.
Oronyi amesema washambuliaji, wanaokadiriwa kuwa kati ya 70 na 100 walifika kwa miguu.
Washambuliaji wa kwanza walipiga mnara wa Kampuni ya Simu ya Safaricom katika mji wa Lafey, kwa lengo la kukata mawasiliano kati ya maofisa na mabosi wao, kabla ya kuvamia kambi hizo.
Amesema askari wa akiba wanaolinda mnara wa mawasiliano walizidiwa na washambuliaji hao waliokuwa na silaha nzito.
"Mnara wa mawasiliano uliokuwa unalindwa na polisi wa akiba ulishambuliwa kwa bomu na ghafla na kukawa hakuna mawasiliano (simu ya mkononi) katika Fino," amesema.Mwananchi
0 comments:
Post a Comment