Sehemu ya wanafunzi wakifuatia jambo katika picha ya maktaba.
Kilomanjaro.Serikali imeifunga Shule ya Sekondari ya Lyamungo kwa zaidi ya wiki mbili baada ya wanafunzi wake kufanya vurugu na uharibifu katika nyumba ya mwalimu wa nidhamu wakipinga mwenzao kufukuzwa.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Onesmo Buswelu amesema lengo la kuifunga shule hiyo ni kuepusha uharibu zaidi na uvunjifu wa amani.
Amesema vurugu hizo zinatokana na mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Moses Siima anayesoma mchepuo wa HGE, anadaiwa kuwatukana walimu jambo ambalo lilisababisha kuadhibiwa pamoja na kusimamishwa masomo.
“Hawa wanafunzi walifanya vurugu na maandamo Februari 28, mwaka huu kwa lengo la kumwona mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kutokana na mwanafunzi mwenzao kuadhibiwa na mwalimu wa Nidhamu wa shule hiyo, Safari Rasini.
“Kamati ya Ulinzi na Usalama, imeridhia wanafunzi wote kuondoka shuleni na wanapaswa kurejea shuleni Machi 18, mwaka huu,” amesema.
WANAFUNZI WABOMOA NYUMBA YA MWALIMU.
Wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Lyamungo iliyopo Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro wamevamia nyumba ya mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo, Safari Mwasile na kufanya uharibifu kwa madai ya kuchoshwa na visa vya mwalimu huyo.
Aidha, wanafunzi hao pia wamefanya uharibifu katika mashamba ya migomba ya shule hiyo huku wakimtaka Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hai kumwondoa mwalimu huyo, na endapo hataondolewa hawakotayari kuendelea na masomo.
Mmoja wa wanafunzi hao amedai chanzo cha mgogoro huo ulitokana na uchaguzi wa viongozi wa shule ambapo katika upigaji kura mmoja mwanafunzi aliandika matusi kwenye karatasi ya kura.
“Baada utambuzi wa hati mwanafunzi aliyeandika matusi hati yake ilibainika na mwanafunzi huyo alipewa adhabu kurudishwa ya nyumbani kwa muda wa wiki mbili,” amesema.
Inadaiwa mwanafunzi huyo aligomea adhabu hiyo ya kufukuzwa shule huku wanafunzi wenzake wakigoma kuingia darasani wakidai kwamba mwalimu wa nidhamu ndiye chanzo cha matusi hayo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment