WABUNGE SITA WALIOPATA AJALI MOROGORO WAWASIRI MUHIMBILI KWA NDEGE
Dar es Salaam. Wabunge sita waliopata ajali jana usiku Machi 29, 2018 mkoani Morogoro wakitokea Dodoma, leo mchana Machi 30, 2018 wamefikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MCL Digital ofisa uhusiano wa MNH, John Masawe amesema wabunge hao wamefikishwa hospitalini hapo saa saba mchana wakitokea Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Amesema kwa sasa wote wapo katika uangalizi wa madaktari na hali zao zinaendelea vizuri.
Amesema miongoni mwao wapo walioumia mikono, vifua na mmoja ameumia kichwani.
Amemtaja aliyeumia kichwani kuwa ni Mbunge wa Makunduchi, Haji Amir Haji. "Huyu ameumia eneo la kichwani ila anaendelea vizuri na vipimo vya CT scan vimechukuliwa kwa ajili ya matibabu zaidi," amesema Masawe.Mwananchi
0 comments:
Post a Comment