BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAPA NDIPO DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOCHEMKA NA NANDY

 

Na Dk Levy.
Ilikuwa ghafla. Ni kama shambulio la kisu ambalo lilipenya mwilini na kuujeruhi moyo wangu. Sikutegemea. Kati ya yote niliyotegemea kuyaona au kusikia Jumamosi ya wiki iliyopita. Niliumia. Unampenda mtu halafu hajui kama unampenda. Inauma sana.

Ilikuwa jioni. Ndipo nilipopata ujumbe wa video kwenye simu kwa njia ya Whatsapp. Video ambayo haikuwa sahihi kuja kwangu. Lakini mtumaji alifanya kusudi. Kusudio lake moyo wangu uvuje machozi ya masikitiko. Nitaeleza punde.

Kwenye moja ya pembe za ukumbi wa Hotel Desderia ndani ya Jiji la Mbeya. Nimekaa. Kinywaji changu mezani chenye vinasaba na utaratibu wa kudhibiti baridi. Wahudumu wengi wao wana maumbile. Sura. Rangi na lafudhi ya Kinyakyusa.

Asubuhi ya siku hiyo nimetoka kumuona gerezani Mbunge wa Mbeya Mjini na mwanamuziki wa kitambo sana, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (mshikaji anawasalimia sana). Simu inajazwa moto ukutani. Macho yangu yako kwenye runinga kubwa ukutani. Habari ni za Syria na makombora ya Marekani.
Mara akatokea mshikaji mmoja ambaye usiku wa jana yake (Ijumaa) alikuwa akinunua vinywaji kwa fujo kuliko mtu mwingine yeyote hotelini hapo, huku akigeuka pedeshee kwa kuwatuza wanamuziki wa bendi iliyokuwa ikiporomosha muziki wa kukopi.

Mpaka siku hiyo mifuko yake bado ilionekana imetuna. Anajichekesha chekesha kwa wahudumu. Akageukia nilipo. Akaniona. Bila salamu akanitandika na kinywaji kingine akimuagiza mhudumu kijeuri na ujivuni. Ni dhahiri kuwa jana yake alinikariri sura.

Mara sauti ya ujumbe mfupi wa Whatsapp ikasikika kwa simu yangu. Nikaichomoa kwenye chaji fasta. Nilikuwa na hamu na mlio wa meseji au simu. Kuna miadi nilipanga na totozi moja ya chuo kikuu hapa mjini. Miadi ya kutengeneza kioo cha simu yake. Napenda sana ufundi wa simu mimi.

Tofauti na nilivyotegemea haukuwa ujumbe wa mrembo yule. Ilikuwa video ya msichana mmoja mwingine mzuri sana. Namzimia kinoma. Kuanzia alivyo kwa sura, umbo, sauti hata rangi yake. Dah. Nilihisi mapigo ya moyo yakienda kasi sana.

Jamaa aliyenitumia video hiyo anajua ni namna gani napenda muziki wa Nandy. Na anajua namuhusudu Nandy. Huwa nakaona kama kamdoli flani hivi amazing. “Video ya utupu? Naaandy... c’mooon!” Sauti ilinitoka bila kujielewa.

Nikainua uso kuona kama watu wamenisikia. Hakuna aliyeniendekeza wahudumu walikuwa bize na yule jamaa aliyenipiga na kinywaji. Wateja ambao tena ndiyo waliokuwa wengi ni Wazungu. Nikainamisha kichwa kuendelea kuangalia kama ni kweli nilichoona.

Nilitamani iwe ndoto. Yaani awe ni msichana wa mbali huko sijui, lakini siyo Nandy.

Jamaa aliyenitumia ile video nikamjibu kuwa “Asante”. Nalo likajibu kwa kicheko kireefu utadhani likicheka sana litapata mgao wa Sh1.5 trilioni. Alinikera. Nandy kaanza safari ya muziki vizuri sana, ni mmoja wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye mapokezi bora. 


Alizaliwa kwa sababu ya muziki. Na muziki upo kwa ajili ya watu kama Nandy. Ni msanii bora sana. Mtoto mzuri mwenye sauti, rangi na umbile yanayoshawishi.

Ni miongoni mwa watoto wa mjini watamu na wabichi, lakini anaharibika ghafla kama nyanya masalo akiwa bado hata hajaona ufalme wa ustaa kwa maana ya ustaa, anaanza kuzingua mapema sana mtoto. Amedata.

Nandy ameamua kuwa Rihanna ghafla wakati hata kuwa Shilole bado. Nandy anaacha kuwaza kuwa Ruby. Anadhani kuwa kapita daraja la Jide. Haya mambo ndiyo yaliyowaondoa kwenye ramani kina Nora.

Ni mtoto, lakini siyo umri wa kuzuiwa kunywa pombe na kuingia kwenye kumbi za starehe. Tatizo siyo kufanya. Tatizo ni kuuonyesha ulimwengu kinachofanywa gizani na watu wa jinsi mbili tofauti. Huu ni udwanzi kama udwanzi mwingine.

Kiki? Hapana siyo kiki. Huu ni wendawazimu tu. Kiki gani za kuwasononesha wazazi? Walezi? Viongozi wako wa kiroho? Waumini wenzako? Majirani? Ndugu jamaa na marafiki huku ukipunguza ushawishi kwa mashabiki?.


Wanachojua wasanii wetu wa sanaa zote na wanajivunia sana ni kupata uchizi baada ya kupata umaarufu na pesa. Kuna akili ya kijinga hujenga urafiki na wao na kuamua kutenda lolote kwa nguvu ya majivuno ya umaarufu.

Wote waliopata kichaa hiki wamefeli kila kitu. Wamefeli kimaisha na kipesa, kiushawishi na kiuhusiano. Yaani hata wapenzi wao walitoweka kwenye mbavu zao.

Inakera. Mungu akupe nini Nandy? Homa ya dengue au matende? Unatafuta kiki kwa video ya matendo ya gizani? Kipi unachokosa kwenye dunia hii ulipofikia? Umaarufu? Usafiri? Lipstick? Make Up? Kope za bandia? Au urojo wa Forodhani kule Zenji? C’moon gal.

Nd’o staa mdogo wa muziki ambaye nilibeti kuwa atakuja kuwa juu kuliko staa yeyote wa kike Bongo. Kila niliposikiliza muziki wake nilikuwa namuona mawinguni, anapaa tu. Mkeka wangu umechanika kabla ‘game’ halijaanza. Yaani timu nd’o kwanza zipo vyumbani.

Kwa aina ya wasimamizi wake wa muziki sidhani kama wamemtuma atende ujinga ule. Kama wamemtuma na Mungu awaumbue na wao watende kama yeye siku za usoni. Ila sidhani.

Ni akili zilezile ambazo leo hii akina Irene Uwoya na Wema Sepetu wanatamani muda urudi nyuma wasitende hayo. Hawa mastaa wetu wengi ambao hii leo wanatamani kuajiriwa na Wasafi TV ni wale ambao wangekuwa na runinga zao kama muda wao wa ustaa wangeutumia vyema.

Nandy ana dada zake wengi ambao wamechemka kimaisha, ambao wanafaa kuwa mfano kwake kukwepa yasimkute yaliyowakuta. Ila ni tofauti. Katikati ya safari Nandy anageuka nyuma. Anarudi njia ileile huku akipita kwenye nyayo za dada zake na mama zake waliofeli.

Anaweza kuchukulia poa kwa sababu hajui madhara yake. Anaweza kuona haina shida kwa sababu kuna mabwege ambao wanajipendekeza kwake kwa kumpa moyo kuwa mbona siyo ishu? Na hao nd’o wengi maana hawana akili.

Hii ni mbaya sana kisanii na kimaisha kwa Nandy. Elizabeth Michael ‘Lulu’ katika makuzi yake alikuwa hivi. Alikuwa anaambiwa hiki na watu wenye akili timamu na mabwege nao wakawa wanamwambia kile. Matokeo yake yako wazi kama vazi la kahaba. Nandy jifunze.

Umesikia ya Diamond? Staa mwenye mji wake. Mwenye nchi yake. Mwenye muziki wake. Mwenye utajiri wake. Mwenye mademu zake ambao anawageuza atakavyo kama chapati. Amerukaruka sana. Amekwenda mbele nyuma, kulia, kati, kushoto na waapi!

Mwisho amegota palepale. Anatazamwa kimataifa, yeye akili yake kaielekeza kitaifa tena, Mwananyamala. Mafanikio ya Diamond ni kwa sababu aliwatazama mastaa wa zamani kama mfano.

Aliangalia nyendo zilizowafelisha akagundua wao walipita kulia yeye akapita kushoto. Ndiyo maana kila kukicha anazidi kuwekeza kwenye maisha, lakini tabia za maisha mengine anapita kulekule walikopita wengi. ‘Any way’ ustaa bila mademu kwa Bongo ni kama Simba bila Yanga.

Tatizo siyo mademu. Tatizo ni kuwadhalilisha. Yawezekana mademu nd’o vilaza. Kwamba wanakwenda wenyewe kwa njaa au sifa za kijinga kwamba niko na Simba toka mbuga ya Tandale. Lakini Diamond mwenye aangalie, yeye ni kioo na balozi wa kampuni nyingi. 


Hizi kiki za kidwanzi za kuachana nazo. Ushawadanganya sana watu kwa kiki hizo huwezi kuendelea kuwadanganya watu wote muda wote. Unaonekana kituko. Nandy na kaka yake Diamond wametoa maboko. Wamefungisha kinoma. Muda siyo rafiki.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: