
Na Geofrey Chambua
Singapori ni marufuku kutafuna Big G au Jojo (ie Chewing Gums) ukibainika faini hadi $1000, itumike kwa sababu za kitabibu tu (Tangu mwaka 2004 kuna Big G maalum zimeruhusiwa kuingizwa nchini humo 'kama dawa').
Pia hairuhusiwi kutema mate chini ovyo. Ukifanya hivyo mara tatu (ukumbuke kuna CCTV Camera) utatakiwa kuvaa bango limeandikwa mimi ni mtema mate ovyo huku unafanya usafi mitaani...........sababu kubwa ni kwamba kuna maambukizi mengi kwenye mate heri ubaki nayo MWENYEWE
2. DENMARK
Huruhusiwi kulipia chakula kwenye mgahawa hadi ushibe. vinginevyo endelea kuagiza hadi ushibe yumkini hata kuvimbiwa maana tabu itakuangukia mwenyewe.
3:UGIRIKI
Polisi wanaruhusiwa kumkamata mtu yoyote anayetuhumiwa/Au hata kushukiwa kuwa na HIV, Wanaweza kukupima HIV kwa lazima na ikiwezekana kukutenga kutoka nyumbani kwako.
4: UFILIPINO NA VATICAN
Nchi pekee duniani ambapo talaka ni haramu (Illegal).
5: INDIA
Kkuna baadhi ya sehemu kama mwanaume anayedaiwa, anamtoa mke wake hadi deni litakapoisha ndio anamchukua...nadhani ndipo asili ya msemo kukopa harusi.
6:HONG KONG.
Mwanamke anaruhusiwa kumuua mume wake akimkamata anacheat/au akigundua anamchepuko. Ila anapaswa kufanya hivyo kwa kutumia mikono yake bila silaha hakuna adhabu ila ni dhambi zako mwenyewe.
7:VICTORIA, AUSTRALIA
Ni kinyume cha sheria kubadili taa/bulb kama sio fundi umeme tena mwenye vyeti halali (Licensed).
8:LEBANON
Kama ukikutwa unafanya mapenzi na mnyama yeyote mwenye jinsi ya Kiume, adhaby yake ni kifungo cha maisha. Ila sheria yao haisemi chochote (silent) kuhusu mnyama wa kike.
9:BANGLADESH
Kama ni mwanafunzi na una umri zaidi ya miaka 15, ukikamatwa unaangalizia (unadesa) unaweza kufungwa jela.
10: GEORGIA......NA ITALY
Iwapo unafuga kuku, ni marufuku kuwaacha wavuke barabara wenyewe (kwani wakigongwa watachafua mazingira-emphasis is mine) ...unatakiwa uwadhibiti kuku wako muda wote, ilihali huko Italy ikiwa unafuga mbwa shuruti umtembeze walau mara tatu kwa siku (yaani uchague kati ya kazi na mbwa)
11. UJERUMANI Ni marufuku Gari lako kuishiwa mafuta njiani kwani ni Kiashiria cha kwamba wewe ni kilaza wa makadirio yaani hukukadiria uwiano wa safari yako na mafuta na adhabu yake ni faini au kifungo
12. KWA AKINA CR7-URENO
Ni marufuku kukojoa (kujisaidia haja ndogo) baharini ama ufukweni, ukishikwa shikamana hadi upate pa kuuhifadhi (japo imekua ngumu kuthibitisha hasa kwa wale wanaosusu baharini)
13. SAUDIA ARABIA
Hakuna umri wa chini (marriage minimum age) wa Binti/mwanamke kuolewa. mwaka 2008, MAHAKAMA ilikataa ombi la kupewa Talaka toka kwa Binti wa Miaka 8 aliyefunga ndoa na Mhenga wa miaka 58
14. ARKANSAS
Ipo sheria ya tangu maka 1800 inayomhalalisha mwanaume kumpiga mkewe japo mara moja tu kwa mwezi na ipo sheria kwamba mwanaume atabebeshwa makosa ama hatia ya mkewe kwa kosa ambalo alilifanya wakiwa pamoja (yaani kosa la mke anaadhibiwa mume)
katika jimbo hili pia ukikosea kuita jina la jimbo ARKANSAS unaweza kushitakiwa
15. UCHINA (Sheria ya Mwaka 2013!!)
Ni marukufuku kuwatembelea wazazi mara kwa mara ukishakua mtu mzima ( umri wa kujitegemea) ....huenda hicho ni kiashiria cha kwenda kupiga mizinga. Nchini Uingereza, ni marufuku kuishi na wazazi baada ya miaka 18.......wameshakupa panga (Elimu) ingia mstuni mwenyewe.
16. FLORIDA.
Ni marufuku kupumua hewa chafu baada ya saa 12 jioni, yaani kama uligonga mkorogo mchana (mchana uligonga karanga, mayai ya kuchemsha, mahindi ya kuchoma, mtindi etc) tafuta KINGA mapema.
Jimbo Honolulu ni marufuku kuimba kwa sauti (kavu kavu) baada ya jua kuzama.
17. SWEDEN
Japo biashara ya ngono ni HALALI (Legal) ni marufuku kukutwa unanunua biashara hiyo (wewe piga kimya tu) maana yake ni kwamba inakula kwa kungwi tu (mnunuzi) sio kwa mwali (muuzaji).. ....Iceland na Norway nazo zimepitisha sheria hii majuzi huenda ni kudhibiti 'FOLENI YA ILALA BOMA'
TANZANIA???
0 comments:
Post a Comment