Afisa Elimu miradi wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) Bi. Alistidia Kamugisha akizungumza kwenye mkutano huo wa wadau.
Elimina Materu na Amina Hezron
Morogoro.
Wito umetolewa kwa jamii kushirikian na vyombo vya habari katika kufichua na kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazochangia kukwamisha maendelea ya elimu kwa wanafunzi nchini.
Wito huo umetolewa Afisa Elimu miradi wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) Bi. Alistidia Kamugisha.
Akizungumza hayo katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro na kusema kuwa bado shule nyingi za msingi na sekondari nchini zinakabiliwa na changamoto mbalimbali.
"Changamoto bado zipo nyingi sana shuleni ikiwepo mimba za utotoni, masuala ya siasa katika utendaji,jamii kutoelewana na kutoshirikiana na uongozi wa shule pamoja na utoro kwa wanafunzi hasa wakati wa kiangazi kwa wakulima na wafugaji jambo linaloonekana kuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya shule zilizo nyingi wilayani humo”,alisema Bi Kamugisha.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Afisa Elimu wa Wilaya ya Mvomero Maajabu Nkamyeka zinasema kuwa mpaka kufikia tarehe 6 ya mwezi huu wilaya imebaini asilimia 90 za mimba za utotoni kwa shule za sekondari pamoja na msingi na asilimia 13 katika shule za msingi na asilimia 77 kwa shule za sekondari.
“Wazazi tukae na binti zetu tuwaeleze ukweli jinsi dunia inavyokwenda kwakuwa unaweza ukahisi labda mtoto wangu ni mdogo hafahamu kitu wakati siku hizi kuna utandawazi mkubwa anaweza akajifunza vitu katika mitandao ya kijamii."alisema Kamugisha.
Aliongeza kwa kusema kuwa ili watoto wasivifanye ni vizuri tukawaweka wazi kuwa unatakiwa kuwa hivi ukifanya hivi utapoteza masomo utapoteza haki yako ya msingi ni vizuri wafahamu hali halisi na wajue matendo yao wanayotenda kipi kizuri kipi kibaya.
Wadau wa elimu kutoka wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakifutilia mkutano huo.
Naye Mkurugenzi kutoka shirika la Safina Womens Association wanaojihusisha na uhamasishaji wa uboreshwaji wa elimu kwa shule za awali hadi sekondari Bi.Hellen Kalangango amesema kuwa wazazi wanalo jukumu kubwa katika kuhakikisha wanawapatia watoto wao haki za msingi kama mavazi, madaftri na malezi bora hali itakayopelekea ufaulu mzuri kwa watoto wao.
"Haya mataamko watu wanafikiri kila kitu ni bure mpaka ulinzi wa shule ni bure lakini kauli ya elimu bure ni kwamba wakati fulani mtoto anatakiwa kuandikishwa kwa kulipia kiasi cha pesa."alisema Blangango.
Aliongeza kuwa kueleza kuwa mwanafunzi kwenda shule na dawati, hayo ndiyo serikali ikaona hapana, wazazi watambue hilo kwa kuwapa watoto wao haki za msingi na siyo kusubiri serikali kuwafanyia kila kitu.
Aidha wazazi wametakiwa kushirikiana na walimu pamoja na vyombo vya sheria katika kuhakikisha watoto wanasoma vizuri na kuripoti kesi za mimba sehemu husika ili kuhakikisha haki ya mtoto inapatikana.
Wadau hao wa elimu wakijadilina kwenye mkutano huo ulioandaliwa na TEN/MET
Mjumbe wa mkutano huo akifurahia jambo wakati wa mkutano
Mjumbe wa mkutano huo bwana Heriamini Mariki akichangia jambo wakati wa mjadala ndani ya mkuatano huo.
0 comments:
Post a Comment