
Real Madrid ilishinda mabao 3-1 huku Gareth Bale akifunga magoli mawili
Real ni timu yenye mafanikio zaidi kwenye historia ya ligi ya mabingwa ikiwa na mataji 13.
Zidane alisema:''hii ni klabu ya wakongwe. Klabu hii imeshinda makombe 13 ya Ulaya nafurahi kuwa sehemu ya historia hii
Aliongeza: '' tunakwenda kufikiria kuhusu tulichokipata, kufurahia wakati huu kwanza.Ni kitu muhimu zaidi kwa sasa''.

Timu tatu pekee zimeshinda kombe la mabingwa barani Ulaya, Real ikiwa na mataji matano tangu mwaka 1956, Ajax (1971-73) na Bayern Munich (1974-76).
Hata hivyo Real ni ya kwanza tangu kubadilishwa kwa jina la michuano hiyo.
Kiungo Luka Modric anaamini itakuwa ngumu kwa timu kufikia mafanikio ya Real''Ni jambo la ajabu la kihistoria, aliiambia BT Sport ''Sijui kama kuna mtu atarudia hili siku za usoni.'
0 comments:
Post a Comment