Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe akimzsikiliza mbunge wa jimbo la Kusini, Omari Mgumba wakati wa ziara ya waziri huyo kushoto kutembelea eneo litakalojengwa bwawa la maji la Kidunda mkoani Morogoro. Picha zote na Juma Mtanda.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe katikati na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Sudi Mpili kushoto wakizungumza mbunge wa jimbo la Morogoro kusini, Omari Mgumba.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe kushoto akimsikiliza Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Mamlaka hiyo, Profesa Felix Mtalo (katikati) wakati wa ziara ya waziri huyo kutembelea eneo litakalojengwa bwawa la maji la Kidunda mkoani Morogoro na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandishi Romanus Mwang’ingo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe akizungumza jambo katika ziara hiyo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe (Mwenye kofia ngumu) akielekezwa jambo na Profesa Filex Mtalo wakati wa ziara hiyo, wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandishi Romanus Mwang’ingo
Kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo, Waziri Kamwelwe (Mwenye kofia ngumu), Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven na Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandishi Romanus Mwang’ingo wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo. Waziri Kamwelwe kulia na Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandishi Romanus Mwang’ingo kushoto wakiondoka eneo la mto Ruvu baada ya waziri huyo kumaliza kukagua eneo hilo litakalo jengwa tuta kwa ajili ya bwawa la maji Kidunda.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven kulia akizungumza na Waziri Isaack Kamwelwe, kushoto ni Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Omari Mgumba.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe kushoto akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandishi Romanus Mwang’ingo (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara wakati wa ziara hiyo.
Meneja Uhusiano Jamii wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Neli Msuya akimweleza jambo Waziri Kamwelwe wakati wakielekea kumuonyesha jiwe lenye alama iliyowekwa mwaka 1967 na wakoloni kama sehemu ya ujenzi wa bwawa hilo. Waziri Kamwelwe wa pili kutoka kushoto akionyeshwa alama ya jiwe (Chini) katika ziara hiyo.
Waziri Mhandisi Kamwelwe akifurahia jambo na Mbunge Mgumba muda mfupi baada ya kumaliza kukagua eneo litakalojengwa bwawa la maji la Kidunda.
Sehemu ya eneo la Kidunda
Mkazi wa Kidunda akisubiria madereva waliokuwa kwenye msafara wa waziri ili kumpata fedha baada ya kutengeneza daraja kutokana na eneo hilo kuwa bovu kutokana na miundombinu ya barabara kuharibika na mvua za masika.
BWAWA LA KIDUNDA MOROGORO MKOMBOZI UPATIKANAJI WA MAJI YA UHAKIKA PWANI, DAR
Na Juma Mtanda, Morogoro.Serikali ipo kwenye hatua nzuri ya kuanza ujenzi wa kujenga bwawa la maji la Kidunda litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji mita za ujazo 190 milioni baada kuvunwa kutokana na mvua za masika ili kuwezesha mitambo ya uzalishaji maji ya mto Ruvu isiteteleke katika kipindi cha mwaka.
Akizungumza na viongozi mbalimbali katika eneo la Kidunda mkoani Morogoro jana, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe alisema kuwa bwawa hilo litakuwa na nyingi ikiwemo kuzalisha umeme, upatikanaji wa maji ya uhakiki kwa wakazi wa Dar es Salaam na viwanda baada ya kukamilika ujenzi wake.
Mhandisi Kamwelwe alisema kuwa moja ya faida ya kwanza bwawa hilo litazalisha umeme wa megawati 20 na kutoa faida ya mitambo ya maji ya Ruvu kuendelea kuzalisha maji mwaka mzima bila kuteteleka kutokana na kupungua kwa kina cha maji vipindi vya kiangazi.
“Serikali imekuwa ikisisitiza kuwekeza sekta ya viwanda na vimekuwa vikitumia zaidi maji hivyo lazima tujipange kwa kutengeneza miundombinu bora ya upatikanaji maji ya uhakika lakini na umeme umekuwa sehemu ya matumizi makubwa kwenye viwanda.”alisema Mhandishi Kamwelwe.
Katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Profesa Felix Mtalo alimweleza, Mhandishi Kamwelwe kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bwawa hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo milioni 190.
Profesa Mtalo alisema kuwa michakato mbalimbali tayari imefanyika ikiwemo kulipa fidia wananchi wa eneo la mradi na upanuzi wa barabara kutoka eneo la barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.
“Michakato mingi imefanyika, Mhe Waziri na iliyobakia ni michache michache ambayo inaendelea kufanyiwa kazi ikiwemo kuhamisha makaburi na mambo mengine ya kitalaamu.”alisema Profesa Mtalo.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandishi Romanus Mwang’ingo alisema kuwa mpaka sasa mamlaka hiyo tayari imelipa fedha za fidia kiasi cha sh11 bilioni kwa wananachi 2603 wa vijiji viwili ili kupisha mradi huo.
Mhandishi Mwang’ingo alisema kuwa wananchi hao waliolipwa fidia wamegawanyika katika makundi mawili ya vijiji na wale waliopisha barabara.
Alitaja vijiji vilivyopisha mradi huo kwa upande wa bwawa kuwa ni Bwila Chini yenye vitongoji vya Kwatupa, Kwagonzi, Vikonge, Kariakoo, Nyagongo na Mnambala huku kijiji cha Kiurumo kikiwa na vitongoji vya Vidwali, Mikoroshini na Mbuyuni.
Kwa upande wa barabara ni pamoja na Matuli, Kwaba, Chanyumbu, Mkulazi na Diguzi.
“Kukamilika kwa ujenzi wa bwawa la Kidunda kutasaidia mitambo ya maji ya Ruvu kufanya kazi kipindi chote cha mwaka maana, kipindi cha kiangazi mto Ruvu umekuwa ukipungua maji na mitambo yake kuwa katika wakati mgumu wa kufanya kazi.”alisema Mhandishi Mwang’ingo.
Mradi wa ujenzi wa bwawa la Kidunda utapoanza utajengwa kwa kipindi cha miaka miatatu hadi kukamilika kwake na bwawa hilo litakuwa na maisha kwa miaka 30 huku likitarajiwa kuwa na uwezo wa kuachiliwa maji mita za ujazo 24 kwa sekunde na kuwezesha mitambo ya maji ya Ruvu kufanya kazi kipindi chote cha mwaka mzima.
0 comments:
Post a Comment