BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAIZER CHIEF FC YASHINDWA KUTAMBA DHIDI YA UHURU RANGERS KATIKA LIGI NDOGO YA TAIFA NGAZI YA MANISPAA YA MOROGORO.

TIMU ya soka ya Kaizer Chief FC imeshindwa kuitambia Uhuru Rangers baada ya kulazimishwa sare wakati wa mchezo wao wa kwanza wa ligi ndogo ya taifa ngazi ya Manispaa ya Morogoro inayoshirikisha timu nne ambazo zimefuzu nusu fainali ya ligi hiyo kwa kufungana bao 1-1 katika harakati za kuwania ubingwa wa wilaya Manispaa ya Morogoro kwa msimu wa mwaka 2011/2012 katika mchezo uliofanyika januari 5 mwaka huu kwenye uwanja wa Sabasaba mjini hapa.

Katika ligi hiyo timu nne zimefuzu kucheza hatua hiyo ni pamoja na Kaizer Chief, Moro Kids U23, Sultan Rangers na Uhuru Rangers ambapo katika ligi hiyo timu ambayo itakuwa imekusanya pointi nyingi ndiyo itayotangazwa kuwa bingwa wa ligi hiyo kwa Manispaa ya Morogoro kwa msimu wa kwa 2011/2012 ambayo itaraji kufika tamati januari 12 mwaka huu.

Katika mchezo huo Kaizer Chief FC ndiyo iliyoonekana kutawala kwa kutandaza soka safi huku wakitumia pasi fupi fupi hali iliyowalazimu Uhuru Rangers kusaka mpira kwa muda mrefu.

Hata hivyo walinzi wa Uhuru Rangers na mlindamlango wao, Isahaka Bene walifanya kazi ya ziada ya kuzuia mashambulizi kutoka kwa washambuliaji wa timu pinzani ili wasilete madhala katika lango lao.

Timu ya Kaizer Chief FC iliendeleza mashambuliki kwa wapinzani wao ambapo katika dakika ya 44 mshambuliaji, Babu Ally aliweza kumzidi ujanja mlinzi wa Uhuru Rangers, Rashid Rashid na kupiga mpira wa juu akiwa eneo la hatari ambao ulimshinda mlindamlango wa timu hiyo, Isahaka Bene na kujaa wavuni na kuandika bao pekee la Kaizer Chief FC katika mchezo huo.

Kwa upande wa Uhuru Rangers iliwachukua hadi dakika 83 kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji, Ibrahim Abdul kufunga kwa njia ya penalti baada ya mlinzi wa Kaizer Chief FC kunawa mpira eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo, Seleman Kinugani kutoa adhabu hiyo na kufanya matokeo kumalizika kwa bao 1-1.

Katika mchezo huo kivutio kikubwa kilikuwa kwa kiungo mshambuliaji wa Kaizer Chief FC, Abuu Amran ambaye aliwahi kuzichezea kubwa za Yanga na Moro United kutokana na uhodari wa kugawa mipira kwa washambuliaji wa timu yake huku ligi hiyo ikitarajia kuzikutanisha timu ya vijana ya Moro Kids U23 dhidi ya Sultan Rangers majira ya saa 10 jioni kwenye uwanja huo wa Sabasaba leo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: