Kikosi cha timu ya CRDB Benki jezi nyeupe na njano ni Taswa FC Morogoro.
Katibu Mtendaji wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro Abeid Dogoli akisalimia wachezaji wa timu ya CRDB Benki
Ramadhaman Libenanga akiwania kuku hata hivyo hakuweza kufanikiwa kumkamata.
Zena Hassan akimaliza mbio za kukimbia na magunia nyumba ya hii picha ni waandishi Idda Mushi kushoto na Hamida Sharif wakati kwa upande wa wanaume ni mshindi Jackson Mbya wa kwanza kushoto na wapi wake ni Ramadhani Libenanga.
Mwanamuziki wa bendi ya Leven Music, Badi Dikule kushoto na Richard maalifa wakitumbuiza wakati wa bonanza la michezo hilo.
TIMU ya soka ya Taswa Fc Morogoro imepoteza mchezo wake dhidi ya timu ya benki ya CRDB Sport Club baada ya kutandikwa kwenye mchezo mkali na kusisimua ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu katika bonanza la michezo la kuaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012 lililoandaliwa na chama cha waandishi wa habari Morogoro (MOROPC) katika uwanja wa Jamhuri kwa bao 2-0 mkoani hapa.
Dalili za kufanya vibaya kwa timu za waandishi wa habari katika bonanza hilo lilianzia katika mchezo wa kukimbiza kuku kwa upande wa wanawake baada ya Chiku Kasika (28) kuibuka mshindi wa kwanza akiwazidi maarifa, Idda Mushi, Hamida Shariff, Latifa Ganzel na Lilian Lucas huku kwa upande wa wanaume Dastan Shekidele akiibuka mshindi pekee kwa waandishi hao baada ya kuwa wa kwanza ambapo washindi wote waliondoka na kuku hao kama zawadi yao kwa ajili ya kitoweo.
Kwenye bonanza hilo wadau mbalimbali walishiriki ambapo katika mchezo wa kukimbia na magunia, Zena Hassan (17) alifanikiwa kuwashinda waandishi wa habari mkoani hapa akiwemo, Idda Mushin na Hamida Shariff kwa kuibuka mshindi wa kwanza wakati kwa upande wa wanaume, Jackson Mboya akiibuka mshindi wa kwanza kwa wanaume katika mbio hizo za kukimbia na magunia ambapo kila mshindi alikabidhiwa zawadi ya sh5,000 na mwenyekiti wa kamati ya bananza hilo, Latif Ganzel.
Kwa upande wa soka hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya Taswa FC Morogoro kukubali kipigo hicho kutoka kwa wapinzani wao ambapo kichapo hicho kilitokana na sehemu ya kiungo kuzidiwa hali iliyotoa mwanya kwa kiungo wa timu ya CRDB SC kutawala mchezo huku ikifanya mashambulizi ya mara kwa mara katika lango lao.
Mshambuliaji wa CRDB SC, Jason Mwenezy alifungua ukurasa wa mabao kwa timu yake kwa kufunga bao la kwanza dakika ya 15 kufuatia krosi ya, Edson Show na kupiga shuti lililomshinda golikipa wa Taswa FC Morogoro huku bao la pili likizamishwa nyavuni na, Aron Methew dakika ya 67 ambapo alilofunga kufuatia kuwalamba chenga walinzi wa Taswa FC Morogoro na kufumua shuti kali lililokwenda moja kwa moja na kufanya mchezo huo CRDB SC kumalizika kwa ushindi wa bao 2-0.
Akizungumzia kipigo hicho kocha wa Taswa FC Morogoro, Peter Kimath alisema timu yake ilicheza vema licha ya kupoteza mchezo huo na kuwa wachezaji wake wameshinda kuzitumia vema nafasi walizopata kwa kupachika mabao wakati wapinzani wao wamepata nafasi mbili na kuzitumia vizuri licha ya timu yake kupata zaidi ya nafasi mbili na kushindwa kuzitumia.
Naye mshambuliaji wa CRDB Sport Club, Jason Mwemezy alisema kuwa katika mchezo huo timu ya Taswa FC Morogoro ilistahili kipigo hicho kutokana na idara ya kiungo kupaya hali iliyowafanya kutawala mchezo kwa muda mrefu na kutengeza mashambuli mengi na kupata mabao hao mawili.
Mwenyekiti wa kamati ya bonanza hilo, Latifa Ganzel alisema bonanza hilo liliandaliwa kwa lengo la kuaga mwaka 2011 na kukaribisha mwaka 2012 ikiwemo kuwakusanya waandishi wa habari ili kuweza kufahamiana huku baada ya kumalizika kwa michezo hiyo viongozi mbalimbali wa serikali na siasa walihudhuria hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Nashera mjini hapa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / BONANZA LA MICHEZO LA KUAGA MWAKA 2011 NA KUKARIBISHA MWAKA 2011 JAMHURI MOROGORO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment