BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KLABU YA MPEPO FC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI YA TAIFA KUWANIA UBINGWA WA MKOA WA MORO 2011/2012.


Mshambuliaji wa klabu ya Mpepo FC, Abdallah Zungu akimtoka mlinzi wa Docks FC, Cleopa Magelewanya wakati wa michezo ya fainali ya ligi ya taifa kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2012 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo katika mchezo huo Mpepo FC walishinda kwa bao 2-1.

Mshambuliaji wa klabu ya Docks FC, Msafiri Juma mbele akitoka pasi kwa mwenzake (hayupo pichani) huku akizongwa na mlinzi wa Mpepo FC, Shabaan Togwa wakati wa michezo ya fainali ya ligi ya taifa kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2012 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo katika mchezo huo Mpepo FC walishinda kwa bao 2-1.

MABINGWA wa soka wilaya ya Kilosa klabu ya Mpepo FC imeendeleza wimbi la ushindi katika mbio za kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2012 baada ya kuitandika Dokcs ya Mvomero katika mchezo mkali wa fainali ya ligi ya taifa mkoa huo kwa bao 2-1 kwenye mfululizo wa michezo hiyo inayoendelea kufanyika uliofanyika majira ya saa 10 jioni kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.

Mpepo FC ambayo imekusanya pointi saba kutokana na kushinda michezo miwili na kutoa sare mchezo mmoja walianza mchezo walilazimika kucheza kufa na kupona baada ya kuanza kufungwa kwa kupachikwa bao 1-0 dakika ya 27 ambalo lilifungwa na mshambuliaji wa Docks FC, Ephahim Moses kwa shuti kali akiwa umbali wa mita 20 na kuingia moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda mlango wa timu ya Mpepo FC, Bembe Kanuti asijue la kufanya.

Baada ya kuingia kwa bao hilo timu ya Mpepo FC walitulia na kucheza soka safi la kufundishwa ambalo lilikuwa na kasi huku wakilishambulizi lango la wapinzani wao ambapo dakika ya 44 mshambuliaji, Nassib Omari aliisawazishia klabu yake kwa bao la kwanza kwa kupiga mpira tiktaka kufuatia walinzi wa Docks FC kuzembea kuondoa mpira eneo la hatari kabla ya kumkuta mfungaji aliyefunga bao hilo hilo la aina yake katika ligi hiyo.

Timu ya Docks FC walishindwa kuendana na kasi ya mchezo huo na kujikuta wakitandikwa bao lingine dakika ya 62 na mshambuliaji, Ally Zungu aliwanyanyua mashabiki wa timu hiyo kwa kufunga bao la pili na ushindi kwa shuti kali akiwa eneo la hatari baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Docks FC na timu yake kuibuka na ushindi huo wa bao 2-1.

Katika mchezo mungine uliowakutanisha timu za Manispaa uliochezwa majira ya saa 8 mchana timu ya Kaizer Chief FC ilifanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza baada ya kuilaza Uhuru Rangers kwa bao 1-0 katika mchezo mkali uliojaa ushindani muda wote wa mchezo.

Kaizer Chief FC walipata bao hilo katika dakika ya 37 ambalo likifungwa na mshambuliaji, Aciry Erias na kuonja ladha ya ushindi ya ligi hiyo baada ya kupoteza michezo miwili ikiwemo mchezo dhidi ya Mkamba Rangers FC waliolala kwa bao 1-0 kwenye ufungu na kuambulia kipigo kingine kutoka kwa timu ya Mpepo FC kwa bao 2-0.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: