Namna dini zinavyohifadhi maandishi ya vitabu vya dini vinapochakaa
Waislam wa Afghanistan wakisoma kitabu kitakatifu cha Quran wakati wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa mtume Mohammad huko Kabul, Afghanistan
Dini kuu tatu zina sheria tofauti juu ya namna ya kutupa nakala zilizochakaa za maandishi ya dini.
Quran haitakiwi kutupwa.
Wayahudi wanaweza kuzika nakala za Torah au wanahifadhi kwenye chumba maalumu. Waroman Katoliki wanaweza kuzika biblia, wakati Waprotestant hawana njia maalumu ya kufanya iwapo inatokea jambo la aina hii.
Maandishi ya dini – yale yanayotokana na maandishi yanayoaminika kutoka kwa neno la Mungu, yana sheria tofauti juu ya wapi na namna ya kutupa maandishi hayo yanapochakaa.
Lakini kile kilichopo kwa wote ni heshima inayoonekana kwenye maandishi hayo, namna ya kutumia kitabu huku ukikishika kama vile kukibusu kitabu hicho ukiwa umekishikilia kwa mikono miwili au kuweka kitabu kingine juu yake.
Nchini Afghanistan, ghasia zilizosababisha mauaji zilitokea baada ya jeshi la Marekani kuteketeza nakala kadhaa za Quran kwa kuzichoma moto.
0 comments:
Post a Comment