VIONGOZI WA MORO PRESS CLUB HAMJAMBO JAMANI.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kushoto akisalimiana na Mratibu wa miradi Moro Press Club, Thadei Hafigwa muda mfupi kabla ya mkuu huyo kufungua mafunzo ya waandishi wa habari ya namna ya kuelimisha umma kuhusu zoezi la vitambulisho vya taifa ambalo litakuwa na lengo la kuweka mfumo wa taifa wa usajili na utambuzi wa watu ambao utasaidia kupata taarifa sahihi za wananchi, wageni na wakimbizi iliyoandaliwa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) mkoani hapa kwenye hoteli ya Nashera, Mwenyekit wa Moro Press Club Aziz Msuya na wapi kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Club hiyo Abeid Dogoli.
HABARI NA JOHN NDITI:
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa ( NIDA) imepanga kukamilisha zoezi la uandikishaji wa kila Mtanzania kuwa na kitambulisho cha Taifa ifikapo Agosti, 2014 kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa 2015, imefahamika.
Katika mkakati huo , NIDA inatarajia kuanza zoezi la kuandikisha umma kuanzia Juni 2012 katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Lindi na Zanzibar baada ya kukamilika kwa maandalizi yake.
Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mamlaka hiyo, Joseph Makani, alibainisha hayo jana mjini hapa
wakati akitoa mada kuhusu historia ya faida za vitambulisho vya Taifa na zoezi la usajili na
utambuzi wa watu kwenye warsha ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro, ambapo
Mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa huo, Joel Bendera.
Tayari utekelezaji wa awamu ya kwanza wa utambuzi na usajili wa wafanyakazi wa Serikali
umekamilika kwa ufanisi mkubwa na hivi sasa NIDA ipo katika hatua ya kutoa vitambulisho
vya awamu ya kwanza Aprili 26, mwaka huu ( 2012) wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za
Muungano.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mamlaka hiyo baada ya kukamilika kwa awamu
ya kwanza, hivi sasa inaingia kwenye awamu ya pili ya usajili wa wananchi , wageni na
wakimbizi kwa Wilaya ya Kilombero na baadaye Mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar.
Pia alisema mbali na maeneo hayo, NIDA itaendelea katika awamu nyingine nchi nzima ili kukamilisha zoezi hilo katika kipindi cha miaka mitatu hatimaye kitambulisho kutumika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Uzalishaji wa NIDA, zoezi hilo ni mtambuka , na ili
kuweza kulifanikisha Mamlaka inafanya kazi kwa karibu na taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Serikali za Mitaa, Rita na Idara ya Uhamiaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina hiyo, pamoja na kupongeza NIDA katika kusimamia mradi wa vitambulisho vya utaifa, ameonya watendaji wa Serikali za vijiji na kata kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika usimamizi wa usajili wa taarifa za awali za wananchi.
0 comments:
Post a Comment