BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MICHEZO YA FAINALI YA LIGI YA TAIFA KUWANIA UBINGWA WA MKOA WA MORO 2011/2012 YAANZA KUTIMUA VUMBI.


Mshambuliaji wa klaby ya Docks FC ya wilaya ya Mvomero, Ephahim Moses kulia akimtoka mchezaji wa The Wailes FC ya wilaya ya Kilombero, Casto Damian chini wakati wa mchezo wa ufunguzi wa fainali ya ligi ya taifa kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2011/2012 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa katika mchezo huo The Wailes ilishinda kwa bao 1-0.


MABINGWA wa soka wilaya ya Kilombero klabu ya Mkamba Rangers FC wameanza vizuri michezo ya ufunguzi ya fainali ya ligi ya taifa ya kuwania bingwa wa mkoa wa Morogoro kwa msimu wa 2011/2012 kwa kuitandika Kaizer Chief katika mchezo mkali na kusisimua mchezo uliofanyika majira ya saa 10 jioni kwa bao 1-0 uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.

Bao pekee la Mkamba Rangers FC lilipatikana dakika ya 74 baada ya mshambuliaji wake Sembus Palis kuunganisha vema mpira wa kona uliochongwa na Salum Matete na kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa klabu ya Kaizer Chief FC, Chaga Malibula na kujaribu kuokoa bila mafanikio na kuandika bao hilo kwa Mkamba Rangers FC.

Kaizer Chief FC wanabidi wajilaumu kwa kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini washambuliaji wake Gabriel John, Elias Azili, Babu Ally na Jerry Katula kushinda kutumia vizuri nafasi walizopata wakiwa eneo la harai kwa kufunga mabao na kupelekea kupoteza mchezo huo.

Nayo klabu ya The Wailes FC ya Kilombero imeanza vema harakati za kuwania ubingwa huo kwa kupata ushindi dhidi ya Docks FC ya Mvomero kufuatia kuilaza kwa bao 1-0 lililopatikana kwa mkwaju wa penalti katika mchezo uliochezwa majira ya saa nane mchana kwenye uwanja huo wa jamhuri.

Mshambuliaji wa The Wailes FC, Edson Kamugisha ndiye aliyepeleka huzuni kwa wapinzani wao kwa kuifungia timu yake bao pekee katika dakika ya 67 baada ya mlinzi wa klaba ya Docks FC kufanya madhambi eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo, Seleman Kinugani kutoa adhabu hiyo ambayo ilizaa bao hilo katika mchezo huo.

Katibu mkuu mtendaji wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) Hamis Semka alisema kuwa ratiba ya michezo ya fainali ya ligi hiyo ambayo ina jumuisha timu sita ikiwemo Mpepo FC kutoka wilaya ya Kilosa, Kaizer Chief na Uhuru Rangers Manispaa wakati wilaya ya Kilombero ikiwakilishwa na Mkambara Rangers FC na The Wailes FC huku Docks FC ikitoka katika wilaya ya Mvomero ambapo kila siku michezo miwili itachezwa ambayo yatafikia tamati machi 3 mwaka huu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: