Mshambuliaji wa Polisi Moro SC Iman Mapunda akitafuta mbinu ya kumfunga mlindamlango wa klabu hiyo Saidi Kawambwa chini wakati wa mazoezi ya mwisho ya klabu hiyo kwenye uwanja wa jamhuri kwa ajili ya ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora itayoanza kutimua vumbi machi 31 ikishirikisha timu tisa mkoani Morogoro.
PAZIA la Ligi Daraja ya Kwanza linafunguliwa leo kwa mchezo kati ya
Rhino Rangers dhidi ya Polisi Dar es Salaam na Trans Camp na Mbeya City
Council kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Ligi hiyo
itashudia kila siku zikichezwa mechi mbili, moja ikianza saa 8 mchana
wakati ya pili ni saa 10 jioni ambapo fainali hiyo itamalizika Aprili 22
mwaka huu kwa timu tatu za kwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
msimu ujao.
Kesho wenyeji Polisi Morogoro watakuwa na kibarua
kizito mbele ya Tanzania Prisons mechi itayochezwa mchana wakati jioni
ni Mgambo Shooting na Mlale JKT.
Akizungumza na gazeti hili
kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro mjini hapa Meneja wa timu hiyo ya
Polisi Moro, Clement Bazo alisema wamejiandaa vya kutosha kuhakikisha
wanashinda mchezo wao wa kwanza ili kujiweka kwenye mazingira mazuri.
Bazo alisema kikosi chake kina kila sababu ya kupata ushindi hapo kesho dhidi ya Prison ya Mbeya.
"Tunawataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuangalia kandanda la kuvutia mchana huo.
ìHii
timu kwa sasa ya kuotea mbali kwani ina mchanganyiko mzuri ya wachezaji
wa polisi na raia hivyo vijana wote wako sawa na tutaanza mbio za
kutafuta nafasi ya timu tatu za kutinga Ligi Kuu msimu ujao,î alisema
Bazo.
Naye Katibu wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) Hamis Semka alisema kuwa baadhi ya timu tayari zimewasili mkoani hapo.
Alitaja
timu hizo kuwa zilizowasili kuwa ni Mbeya City, Tanzania Prison na
Mgambo Shooting ambazo zilifika katika mji huo mapema huku nyingine
zikitarajia kuwasili jana na leo.
Ratiba ya ligi hiyo inaonyesha
mechi ya pili siku ya ufunguzi itakuwa kati ya Trans Camp na Mbeya City
Council. Kesho ni Tanzania Prisons na Polisi Morogoro zitakazocheza
mchana wakati jioni ni Mgambo Shooting na Mlale JKT.
Jumatatu
Aprili 2, Polisi Tabora vs Rhino Rangers (mchana) na Polisi Dar es
Salaam vs Trans Camp (jioni). Aprili 3, ni Mbeya City Council vs
Tanzania Prisons (mchana) na Polisi Morogoro vs Mgambo Shooting (jioni).
Aprili 5, ni Polisi Tabora vs Mlale JKT (mchana) wakati jioni
ni Rhino Rangers vs Trans Camp. Aprili 6 mwaka huu Polisi Dar es Salaam
vs Mbeya City Council (mchana) wakati jioni ni Tanzania Prisons vs
Mgambo Shooting.
Aprili 8, ni Mlale JKT vs Polisi Morogoro
(mchana) wakati jioni itakuwa Polisi Tabora vs Polisi Dar es Salaam.
Aprili 9, ni Mgambo Shooting vs Rhino Rangers (mchana) wakati jioni ni
Trans Camp vs Tanzania Prisons.
Aprili 11, ni Mbeya City Council
vs Polisi Tabora (mchana) na Mlale JKT vs Rhino Rangers (jioni). Aprili
12, Polisi Dar es Salaam vs Mgambo Shooting (mchana) na Polisi Morogoro
vs Trans Camp (jioni).
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment