BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DC ULANGA:TUKIO LA MAUAJI YA RAIA WATANO JAMII YA WASUKUMA WALIOPIGWA RISASI NA KUPOTEZA MAISHA NI TUKIO LA KAWAIDA KAMA MATUKIO MENGINE YANAYOTOKEA HAPA NCHINI.


MKUU WA WILAYA YA ULANGA FRANCIS MITI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA WANAHARAKATI WA MITANDAO YA MASHIRIKA YANAYOTETEA HAKI ZA ARDHI NA WAZALISHAJI WADOGO NA WAFUGAJI WA ASILI TANZANIA (TALA)MARA BAADA YA KIKOSI HICHO KUFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA YATIMA, WAFIWA NA KUFANYA MAHOJIANO YA KINA KWA WATU WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO ENEO LA MAGUBA KIJIJI CHA KIWALE TARAJA YA MALINYI HIVI KARIBUNI MKOANI MOROGORO.
BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI NA WANAHARAKATI WA MITANDAO YA MASHIRIKA YANAYOTETEA HAKI ZA ARDHI NA WAZALISHAJI WADOGO NA WAFUGAJI WA ASILI TANZANIA (TALA) WAKIMJULIA HALI MZEE MSHESHIWA NDAHYA (52) AKIUGUZA JERAHA KATIKA GOTI BAADA YA KUDAIWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) ENEO LA MAGUBA AMBAPO KATIKA TUKIO HILO WATU WATANO WALIFARIKI DUNIA NA WATATU KUJERUHIWA NA RISASI AKIWA KATIKA HOSPITALI YA LUGALA LUTHERANI MALINYI HIVI KARIBUNI.


HABARI KALIMI BAADA YA MAHOJIANO YA KINA NA WAKUU MBALIMBALI JUU YA TUKIO LA KUSIKITISHA LA MAUAJI MALINYI ULANGA.

MAUAJI ya watu watano wa jamii ya kisukuma yaliyodaiwa kupigwa risasi na mwanajeshi wa jeshila wananchi wa Tanzania (JWTZ) Koplo Paul Lawlent mwenye namba MT70328 ambaye nimsaidizi wa mshauri wakati kikosi cha doria cha wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro yameibua maswali mengi hukumkuu wa wilaya hiyo, Francis Miti, akieleza sababu nne zilizosababisha mauajihayo na kuwa tukio hilo ni tukio la kawaida kama matukio mengine yanayokea hapanchini.

Tukio hilo ambalo lilitokea Machi 17, mwaka huu limeibuamaswali mengi kuliko majibu hasa kutokana na kuhusika kwa mwanajeshi wa jeshila wananchi wa Tanzania (JWTZ) Koplo Paul Lawlent mwenye namba MT70328 ambaye nimsaidizi wa mshauri wa mgambo wilaya ya Ulanga na matumizi ya risasi za motokatika tukio hilo.

Mkuu wa wilaya hiyo katika mahojiano yake na waandishiwa habari na wanaharaka wa mitandao ya Mashirika yanayotetea haki zaardhi kwa wazalishaji wadogo na wafugaji wa asili Tanzania (TALA) alisema kuwa maamuzi ya kikosi cha dolia kufyatua risasi na kuwauawatu hao yalitokana na madai ya sababu nne ambazo ni pamoja na tishio lawananachi wa kitongoji cha Lubemende katika kijiji cha Kiwale eneo laMaguba tarafa ya Malinyi mkoani Morogoro la kuwavamia na kutaka kuwanyang’anyasiraha waliyokuwanayo.

Hali hiyo iliwalazimu askari wawili wa jeshi lawananchi, wanamgambo tisa na walinzi wawili wa mazingira katika eneo la oevu kufyatuarisasi baridi kwa lengo la kuwatisha lakini baada ya kuona wananchi haohawatishiki walilazimika kutumia siraha za moto zilizosababisha vifo hivyo ambapo watu wengine watatu wakiaachwa na vilema vya kudumu kwa kupigwa na risasi miguuni.

Waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na LutalaNdahya (45), Sanyiwa Ndahya (28), Kashinje Msheshiwa (35), Ng’erebende Lukeresha(26) na Kulwa Lukubije (25), ambapo kati yao watatu wanatoka katika familiamoja ya Ndahya ambao walizikwa katika eneo moja la Maguba katika kitongoji chaLubemende kijiji cha Kiwale.

Majeruhi wa tukio hilo ni pamoja na Msheshiwa Ndahya(52) aliyepigwa risasi katika goti la mguu wa kulia, Zina Msheshiwa (29)akijeruhiwa katika goti la mguu wake wa kushoto na wote wamelazwa katikahospitali ya Lugala Lutheran Malinyi kwa ajili ya matibabu.

Miti alisema kuwa tukio la kupigwa risasi kwa raiaambao ni wakulima na wafugaji wa jamii ya wasukuma eneo la Maguba kuwa ni tukiohilo ni tukio la kawaida na kueleza kuwa kama matukio mengine yanayotokealikiwemo la wasanii wa kundi la taarabu la FiveStars ambao walifariki duniakatika ajali ya barabarani  ndani ya hifadhiya taifa ya Mikumi mwaka jana.

“Hili tukioni tukio la kawaida kama matukio mengine yanayotokea hapa nchini kama lile lawasanii wa kundi la taarabu la FiveStars ambao walifariki dunia katika hifadhiya taifa ya Mikumi.
“Hii jamani haikuwa operesheni bali ni doria yakawaida tu ambayo hufanywa kila mara kwa mwezi mara mbili ama mara  tatu katika hifadhi katika vitalu vyauwindishaji vya Kilombero Game Controlled na kitalu cha uwindaji cha kampuni yaShalom kwa lengo la kuimalisha ulinzi.” alisema Miti.

Katika hatua nyingine alisema kuwa halmashauri mweziAgosti mwaka huu inatarajia kufanya operesheni ya kuwaondoa wakulima nawafugaji waliopo ndani ya hifadhi na katika vitalu vya uwindishaji na kwambatayari halmashauri hiyo imeomba msaada kutoka serikalini huku akibainisha kuwaoperesheni hiyo itahusisha makundi mengine wakiwemo askari wa jeshi la polisi,waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu na wengineo ili kuangaliazoezi hilo litavyoendeshwa bila unyanyasaji kwa wafugaji na wakulima.

Akibainisha zaidi juu ya msafara huo wa doriakushirikisha askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania na mgambo Miti alisemakuwa katika msafara huo hafahammu ila uliratibiwa na idara ya ardhi, maliasilina mazingira wilaya hiyo na kuwa yeye hawezi kuingilia kazi za idara nyinginekwani kila shughuli za kila idara husika zina mamlaka ya kupanga ratiba zake.

Mkuu huyo ambaye ni mwenyekiti wa ulinzi na usalamawilaya ya Ulanga alisema kwa sasa anasubiri taarifa ya uchunguzi wa tukio hilona kuwa bado hajafahamu kama tukio hilo limetokea ndani ya hifadhi ama laakwani kutokana na utata huo tayari ameagiza wataalamu mbalimbali ndani yahalamshauri ambao watafanya kazi ya uchunguzi ikiwemo kutambua eneo husika latukio ili kufahamu ukweli huo na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waliohusikana tukio hilo la mauaji hayo.

NAYE Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro AdolphinaChialo akitoa taarifa za tukio hilo mbele ya waandishi wa habari na wanaharakawa mitandao ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya kutetea haki za ardhi Tanzania(TALA) alisema jeshi la polisi linawashikilia watu 15 wakiwemo wanajeshi wawiliwa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ), mgambo tisa, askari wawili wa vijiji wamazingira na dereva mmoja.
 
Akiongea ofisini kwake Chialo alisema kuwa mpakasasa jeshi la polisi linawashikilia watu 15 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji yawatu watano katika kijiji cha Kiwale tarafa ya Malinyi eneo la Maguba baada yakutokea mauaji machi 17 mwaka huu katika wilaya ya Ulanga mkoani hapa.
 
Chialo aliwataja wanajeshi hao kuwa ni mshauri wamgambo wilaya ya Ulanga, Job Edward Matonya na msaizidi wake koplo, PaulLawlent, mgambo tisa na askari wa kulinda mazingira kutoka katika vijiji viwiliakiwemo na dereva wa halmashauri, Omari Mtua katika kituo kikuu cha polisi mkoa huo huku uchunguzi wa tukio hilolikiendelea na baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo watafikishwa kwenye vyombovya sheria.
 
Kwa mujibu wa kamanda huyo alisema kuwa machi 17mwaka huu koplo Paul Lawlent akiwa na bunduki aina ya SMG yenye namba1775SW02962 mali ya jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wenzake wakiwakatika doria eneo la Maguba walifyatua risasi na kuua watu tano na kuwajeruhiwatatu kwa risasi za moto baada ya kutokea vurugu kati yao dhidi ya wakulima nawafugaji wa jamii ya wasukuma wa kitongoji cha Lubemende eneo la Maguba tarafaya Malinyi wilayani Ulanga mkoa hapa.

Alisema wakati wakiendelea na kazi hiyo kundi lawafugaji na wakulima walidaiwa kuwavamia kundi hilo jambo ambalo walilazimikakufyatua risasi za baridi kabla ya kufyatua risasi za moto ambazo ziliwajeruhiwatu nane kati yao watano walifariki dunia na kujeruhi watatu ambao wawili wamelazwakatika hospitali ya Lugala Malinyi na mmoja ameruhiwa baada ya kupigwa risasikatika nyama za paja.
 
Katika tukio hilo koplo Paul Lawlent alijeruhiwakichwani kwa kupigwa na fimbo ambapo kwa upande wa wafugaji Msheshiwa Ndahya(52) alipigwa risasi katika goti la mguu wa kulia, Zina Msheshiwa (29)akijeruhiwa katika goti mguu wa kushoto huku Chisongile Tiga (30) akiwaamejeruhiwa kwenye nyama za paja mguu wa kushoto ambaye alipatiwa matibabu nakuruhusiwa baada ya matibabu.
 
UMOJA wa Wafugaji Kanda ya Mashariki (UWAKAMA) umesikitishwakutokea kwa tukio la mauaji ya raia watano waliopigwa risasi na wengine watatu kujeruhiwabaada ya kudaiwa kufanywa na askari wa jeshi la JWTZ katika kitongoji chaMaguba kijiji cha Kiwale tarafa ya Malinyi wilaya ya Ulanga hivi karibuni mkoanihapa.

Makamu Mwenyekiti wa umoja huo Masasila Kabisa aliliambiagazeti la mwananchi katika tarafa ya Malinyi kuwa kuwa umoja huo umesikitishwakutokea kwa tukio hilona kuwa nguvu iliyotumika ni kubwa mno ukilinganisha na maafa yaliyotokea ikiwemowahanga kuwaachia vilema vya maisha.

Kabisi alisema kuwa kwa taarifa za chanzo cha mauaji hayoalizonazo zimesababishwa na askari jeshi hao ambao walianza kupora mifugoikiwemo kuku siku ya machi 17 majira ya saa 5 asubuhi ambao walitumia kamachakula kabla ya kuanza operesheni ya kukamata mifugo (ng’ombe) wasiozidi 30katika eneo hilobila ya kuwashirikisha viongozi na wazee wa kitongoji hicho cha Maguba.

Katika idadi hiyo ya watu watano ambao wamefariki dunia kwakupigwa risasi ni pamoja ya Lutala Ndahya (45) aliyepigwa sehemu ya Kichwani nakiunoni, Sanyiwa Ndahya (28) eneo la kifuani, Kashinje Msheshiwa (35) katikaeneo la tumbo wakati Ng’erebende Lukeresha (26) akiwa amepigwa katika eneo lambavu na paji la uso huku Kulwa Lukubije (25) huyu akiwa mtu wa kwanza kupotezamaisha katika tukio, alisema Lukubije.

Maiti watatu wa ukoo wa Ndahya zilizikwa katika eneo la Magubamchangani akiwemo kijiji cha Kiwale kata ya Igawa ni Sanyiwa Ndahya, KashinjeMsheshiwa na Lutala Ndahya waliozikwa machi 18 wakati Kulwa Lukubije naNg’erebende Lukeresha machi 19 mwaka huu walizikwa katika kitongoji hicho.
“Nguvu iliyotumika ni kubwa sana na taarifa nilizonazo chanzo cha mauajihaya yamesababishwa na wanajeshi ambao waliwajeruhi raia wa jamii ya kisukumakwa risasi kabla ya wananchi hao kujaribuni kupambana nao hila ya mafanikio”alisema Kabisi.

Makamau Mwenyekiti huyo aliendelea kueleza kuwa kabla yakufika katika kitongoji hicho cha Maguba kijiji cha Kiwale wanajeshi hao pamojana mgambo walipora mali za wafugaji katika vijiji vya Ipela na Itete ikiwemo navitongoji vya Mpululu na Nganawa vilivyopo ambapo wenye mifuho mingi walitozwafaini ya fedha kiasi cha sh 1.5Mil hadi sh 2Mil na wenye mifugo michache wenyewapigwa fainai ya ng’ombe mmoja sh 10,000 ambapo vijiji hivyo na vitongoji vimokando ya hifadhi ya Maguba.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: