Mshambuliaji wa JKT Mlale Edward Malimi kushoto akimtoka mlinzi wa Polisi Tabora Rajabu Mlindwa wakati wa ligi daraaja la kwanza hatua ya tisa bora katika michezo inayoendelea kufanyika kwenye uwanja wa Jmahuri mkoani Morogoro katika mchezo huo JKT Mlale ilishinda kwa bao 2-1.
KLABU ya JKT Mlale imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza mara baada ya kuitandika Polisi Tabora kwa bao 2-1 huku Rhino Rangers nayo ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 kwa kuitambia Transit Cam katika michezo inayoendelea ya ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
JKT Mlale ilipata mabao yake mawili kupitia kwa kwa washambuliaji Hamis Kisusi na Edward Malimi katika dakika ya 5 na 10 kipindi cha kwanza wakati lile la Polisi Tabora lilipachikwa wavuni na Renatus Severin dakika ya 66 akimalizia pasi ya kifuani ya mshambuliaji Lameck Bundala.
Kisusi bao lake kwa shuti la umbali wa mita 20 akimalizia pasi ya Omari Mnubi naye Malimi akifunga bao la pili la Mlale kwa kugongeana pasi na Igogo Maganga na kupiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Katika mchezo wa pili Rhino Rangers FC ilipata bao lake kuongoza dakika ya 16 kupitia kwa mshambuliaji Amri Sambiga aliyeunganisha krosi ya Venance Genda na kufungwa kwa kichwa na kumwacha mlinda mlango wa wa Transit Camp Batazal Raphael asijue la kufanya.
Julius Masunga aliikosesha bao Rhino dakika ya 46 baada ya mkwaju wa penalti kutoka nje sentimeta chache kutoka kwenye lango kufuatia mlinzi wa Transit Camp kufanya madhambi kwa mchezea vibaya, Mrisho Mnubi katika eneo la hatari na mwamuzi kutoka Mwanza Allonus Luwena kutoa adhabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment