Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdulaziz Abood kulia na Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Francis Lugamala wakiangalia katapili likisawazisha kifusi katika barabara kuu ya Nanenane-Kichangani inatengezwa kwa kiwango cha changalawe wakati wa ziara ya mbunge huyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara zote zinazojengwa kwa kwa kiwango cha lami na changalawe na halmashauri hiyo ambazo zinakadiliwa kutumika kiasi cha sh 510.4Mil mkoani hapa jana.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdulaziz Abood (mwenye kaunda suti) na Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Francis Lugamala wa pili yake kulia sambamba na msafara wake wakimwangilia fundi ujenzi Lucas Michael akijenga kingo za daraja la Mwere lililopo katika kata ya Kingo ambalo kukamilika kwake litasaidia kupunguza foleni ya magari katika barabara ya Old Dar es Salaam ndani ya Manispaa hiyo.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdulaziz Abood kulia akifafanua jambo kwa Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Francis Lugamala (katikati) na Mwenyekiti wa mtaa wa Nkomo kata ya Kingo Manispaa ya Morogoro, Ahmad Bongisa wakati wa ziara hiyo.
NA, ESTHER MWIMBULA.
HALMASHAURI ya manispaa ya Morogoro imetakiwa kuboresha miundo mbinu mbalimbali ya soko la kikundi lililopo katika kata ya kikundi katika Manispaa hiyo ili liweze kutumiwa na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga wanaohamishiwa kutoka sehemu mbalimbali zisizo rasimi
Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Abudulaziz Abood alisema kuwa halimashauri ya morogoro katika zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara ndogondogo toka katika maeneo yasiyo rasimi kwenda eneo la soko la kikundi lilopo mjini hapa lazimu iboreshe miundo mbinu muhimu ikiwemo ujenzi wa vyoo,mifereji ya maji na kuwepo kwa kituo kidogo cha daladala ili kuwawezesha wateja kwenda eneo hilo.
Alisema kuwa endapo miundo mbinu itaboreshwa katika eneo hilo itakuwa rahisi kwa kundi hilo la wafanyabiashara ndogondogo kuhamishiwa hapo kutokana na zoezi hilo awali lilishindika kuhamia eneo hilo kutokana na halmashauri hiyo kushindwa kukidhi viwango hivyo na kuwafanya kurudi tena mitaani.
Pia alisema kuwa kundi hilo la wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga ni muhimu katika kuchangia pato la taifa na kujiingiza katika soko la ajira binafsi hivyo kuchangia kuondokana na tatizo la umasikini kwa kujiongezea kipato.
Aidha alisema kuwa ni muhimu kwa halmashauri ya manispaa ya morogoro kuboresha mazingira ya kufanyia biashara katika eneo hilo iliwaweze kuwasaidia wafanya biashara wadogowadogo amabo idadi kubwa ni wanawake amabo wamejikita katika shughuli hizo ili waweze kuondokana na dhana potofu kuwa kuwa wanaweke tegemezi katika familia zao.
Hivyo aliitaka halmashauri hiyo kuboresha miundo mbinu ya soko hilo ndipo wawaamishe wafanya biashara hao kwani sehemu yeyote ya biashara inatakiwa kuwa na huduma muhimu ikiwemo vyoo, maji, na kuboresha maeneo ya soko .
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo mfanya biashara ndogondogo anaye jishughulisha na biashara ya viatu katika soko hilo Juma Ndeka alisema kuwa wamekuwa wakifanya biashara kwa mazingira kutokana na halmashauri kulitelekeza eneo hilo ambalo halijaandaliwa kuwa soko hivyo kuwafanya wateja kushindwa kwenda eneo hilo.
Pia alisema kuwa licha ya halmashauri hiyo kupanga siku za mnada siku ya jumamosi bado wateja wamekuwa hawafiki katika soko hilo hivyo kuwafanya wafanya biashara hao kupata hasara kutokana na kuuza vitu bei ambayo haiwakidhi katika kuhudumia familia zao ikiwemo karo ya shule.
KATIKA hatua nyingine Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Morogoro imetenga jumla ya shilingi 414Bil kwa ajili ya ukarabati wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo utengeneza ji wa barabara kwa kiwango cha lami kwa baadhi ya barabara zilizopo katika manispaa hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkandarasi wa manispaa ya Morogoro Francis Rugemalila anaye jenga barabara za kiwango cha lami na ujenzi wa daraja la mwere ambalo lipo katia hatua zamwisho alisema kuwa halmashauri imetumi gharama hiyo kwaajili ya kuboresha miundo mbinu ya halmashauri hiyo.
Rugemalila alisema kuwa halmashauri ya manispaa ya Morogoro imejiwekea utaratibu wa kukarabati miundo mbinu ya halmashauri hiyo kila bada ya mwaka mmoja wanafanya ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilometa 2 na kuhakikisha barabara zote zinafanyiwa ukarabati.
Alisema kuuwa ukarabati mwingine utafahusu kukarabati mifereji yailiyo zunguka manispaa ya morogoro ili kuboresha muonekano wa mazingira na kuboresha miundo mbinu ya manispaa hiyo.
Alisema kuwa batabara zinazojengwa katika manispaa hiyo ni zakiwango kikubwa ambapo alisema kuwa magari yanayo beba mizigo inayo zidi tani kumi hayatoruhusiwa kubita katika barabarahizo kwani zitakapo toa kibali cha kupita magari hayo barabara haito kuwa imara .
Aidha alisema kuwa madereva wa magari yanayo beba mizigo chini ya kiwango cha barabara hizo wasipitishe magari yao kwani kufanya hivyo watasababisha kuharibika kwa barabara hizo pindi zitakapo anza kutumiwa rasmi na manispaa hiyo.
Alisema kuwa barabara zinazo jengwa kwa kiwango cha lami ni barabara ya kikundi, bundi, konga, Madaraka, mbago, mazimbu, Tubuyu, na kilakala sekondari ndizo zinanufaika na ukarabadi huo kwa kiwango cha lami.
0 comments:
Post a Comment