BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIUNGO WA KLABU YA AZAM, RAMADHAN CHOMBO AELEZA KUWA KIFO CHA MAFISANGO NI PIGO KUBWA.

 Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akitoa heshima za mwisho wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu, Patrick Mafisango.
 Mlezi wa klabu ya simba, Prof. Philimon Sarungi akimfariji Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage kushoto.
KIUNGOWA MSHAMBULIAJI WA SIMBA  HAROUN MOSHI (BOBAN).

KIUNGO wa Azam, Ramadhani Chombo 'Redondo' amesema kifo cha Patrick Mafisango ni pigo kubwa kwake kutokana ndiye alimtaka aondoke Maisha Club ili akalale muda mfupi kabla ya kifo chake.

Redondo aliyekuwa na marehemu Mafisango kwenye ukumbi wa Maisha Club hadi saa 7 usiku ambako Mafisango alimtaka aondoke kwa madai kuwa muda ulikuwa umekwisha.

Akizungumza kwa shida kutokana na kuelemewa na uzito wa msiba huo alisema haelewi ni nini kimetokea na kwa nini alimfukuza pengine wangekuwa wote kwenye safari ya kurudi.

"Tulikuwa wote hadi mwisho kwenye ukumbi wa maisha klabu, lakini ilipofika muda ya saa saba nane kasorobo  Mafisango alinifukuza na kunichukulia taxi nirudi nyumbani na kuniaambia muda umeisha yeye atarudi na jamaa zake ambao alikuwa nao akiwemo mtoto wa dada yake,"alisema na kuongeza

"Nilikubali nikaondoka cha kushangaza napata taarifa alfajiri kuwa Mafisango amefariki Mungu amefanya kazi yake kumchukua, lakini mimi imeniathiri kutokana na mambo mengi niliyoongea nae"alisema na kushindwa kuendelea kuongea.

Alifafanuwa kuwa aliongea mambo mengi na Mafisango ambayo akiyakumbuka haamini kilichotokea, na bado haelewi nini aseme kuhusu kifo hiki cha ghafla cha rafiki yake huyo.

Tangu kutokea kwa msiba huo Redondo amekuwa hajielewi na muda mwingi anakuwa kama amezimia ingawa baadae hurudi kwenye hali ya kawaida.

Wakati huohuo; Kwa siku ya pili mfululizo kiungo wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' ameendelea kuwa 'Bubu' huku akilia muda wote kufuatia msiba wa swahiba wake Patrick  Mafisango.

Boban aliyeguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huo tangu kufariki kwa mchezaji huyo amekuwa katika hali isiyo ya kawaida huku akikataa kabisa kuzungumza na mtu na muda wote akionekana mwenye huzuni kubwa na machozi yakimtoka mfululizo.

Wakati taratibu za kusoma risala kwa watu mbalimbali zikiendelea Boban alishindwa kujizuia na kuinuka kutoka alipokuwa amekaa na kwenda moja kwa moja karibu na jeneza na kukaa chini huku akilia na kushindwa kuzungumza lolote mpaka alipoletewa kiti.

Aidha baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa waliiambia Mwananchi jana kuwa Boban hakuwa katika hali nzuri tangu aliposikia kifo cha Mafisango ambaye wamedai alikuwa wawili hao walikuwa ni zaidi ya rafiki kutokana na ukaribu wao wakati wote akiwa hapa nchini.

"Tangu tukio litokee Boban amekua katika hali hii hii na amekua hazungumzi lolote, hivi tunavyokwambia asubuhi ameamka akaja moja kwa moja bila kuaga mtu na amekuja huku bila ya viatu 'pekupeku' hata mswaki hakupiga tulichofanya ni kumnunulia viatu na tumejaribu kuwa naye karibu ili kumwondolea hali hii," walisema wachezaji wenzake.

Boban ndiye mchezaji aliyependekezwa kwenda kumzika Patric Mafisango jijini Kinshasa,Congo ambapo anataraji kuondoka leo alfajiri na mwili pamoja na baadhi ya viongozi wa Simba ambao wataambatana pamoja.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: