BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHADEMA V/S POLISI ILIKUWA HAPATOSHI KATIKA MJI KASORO BAHARI, MMOJA AFARIKI DUNIA AKIDAIWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI WA JESHI LA POLISI.

 Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akiongoza umati  uliohudhuria mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) baada ya mtu mmoja kudaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia wakati wengine wawili nao wakidaiwa kujeruhiwa kwa kupigwa na risasi na askari wa jeshi la polisi.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 asubuhi eneo la Msamvu barabara kuu Dar es Salaam-Morogoro wakati askari hao wakiwatawanya umati mkubwa wa wanachama na wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakisubiri viongozi wa juu wa chama hicho ili waandamane kuelekea katika mkutano wa hadhara uwanja wa Ndege mkoani Morogoro leo. 
 Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akihutubia wananchi wa Manispaa ya Morogoro katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ndege mkoani Morogoro. 
 Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliojitokeza katika mkutano huo. 
 Mbunge wa viti MaalumChadema Suzan Mungi akimwaga sera za chama hicho.
 Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar Said Issa Mohamed akifafanua jambo kwa wananchi hao.
 Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Igunda kupitia Chadema, Joseph Kashinde akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
 Mbunge wa jimbo la Ubungo Jijini Dar es Salaam John Mnyika akipanda jukwaani wakati akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Sehemu ya umati ambao ni wakazi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake katika mkutano huo. 

SHUGHULI YA WANACHADEMA ILIPOINGIA DOSARI BAADA YA ASKARI KUWATAWANYA KWA KUPIGA MABOMU NA KUKAMATA BAADHI YA VIONGOZI WALIOKUWA NA WANACHAMA NA WAFUASI  HAO ILI KUWEZA KUPOKEA MSAFARA WA KATIBU MKUU DK SLAA NA VIONGOZI WENGINE ENEO LA MSAMVU.
Mkuu wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) BENSON KIGAIYA akiwa chini ya ulinzi wa gari la polisi mara baada ya kukamatwa wakati wa zoezi la kuwapokea viongozi wa juu wa chama hicho kushindikana katika eneo la Msamvu kwa ajili ya maandamano kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema shule ya msingi Uwanja wa Ndege mkoani Morogoro.
Mama na mtoto, uchungu wa mwana aujuae mzazi, hapo kila mtu aliweza namna ya kujisalimisha na moshi wa mabomu baada ya kupigwa.
 Askari akikimbilia gari baada ya kuanza kwa ufyatuaji wa mabomu katika eneo hilo
 Boda Boda akimpa maji mtoto wa kike ili aweze kunawe kupunguza moshi wa mabomu yaliyopigwa na askari wa FFU wakati wakitawanya wanachadema ili wasiandamane katika kituo cha mafuta cha BP Msamvu.
 Huyu naye alikuwa akitembea huku gari la FFU likiwa nyuma yake baada ya kupigwa kwa mabomu eneo hilo la Msamvu.
 Mmoja wa kiongozi wa Chadema akitiwa nguvuni wakati wa maandamano hayo yanaendelea wakati wakielekea katika uwanja wa shule ya Kiwanja cha Ndege.
 Hawa liingia kwa namna yake huku wakiwa na bango wakiingia kwenye uwanja huo baada ya askari wa jeshi la polisi kufanikiwa kuvunja maandano kwa baadhi ya makundi ya wanachadema.
Mfuasi wa Chadema akiwa na bango wakati akiingia katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndegea kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa M4C.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: