RISALA za rambirambi zinaendelea kutolewa kufutia kifo cha mtu
wa kwanza kufika mwezini, mwana anga wa Marekani Neil Armstrong.
Armstrong mwenye umri wa miaka 82, alifariki kutokana na matatizo ya
moyo
Armstrong alisema kwamba alichokifanya, ilikuwa ni hatua fupi kwake
kama binadamu mmoja, lakini ilikuwa ni hatua ndefu mbele, kwa binadamu
wote duniani.
Alikuwa kamanda wa kikosi cha safari ya Apollo 11 - pamoja na
mwanaanga mwengine Buzz Aldrin.
Mamilioni ya watu duniani kote waliweza
kufuatilia kwenye televisheni mnamo mwaka wa 1969, jinsi Armstrong
alivyotua mwezini, umbali wa kilometa 400,000 kutoka kwenye sayari ya
dunia.
Armstrong alisema wakati huo kwamba alichokifanya, ilikuwa ni hatua
fupi kwake kama binadamu mmoja, lakini ilikuwa ni hatua ndefu mbele, kwa
binadamu wote duniani.
Rais Barack Obama amemsifu mwanaanga huyo kuwa
ni shujaa mkubwa kabisa wa Marekani ambae kamwe hatasahaulika.
Armstrong aliefariki kutokana na matatizo yaliyoyababishwa na maradhi
ya moyo, baada ya kuifanyiwa upasuaji mapema mwezi huu, amesifiwa kwa
utayarifu wa kuzikabili na kuzishinda changamoto zilizoonekana kutoweza
kushindika.
Rais Obama aliyasema hayo wakati akiongoza katika
kuwasilisha rambirambi pamoja na mwanaanga Buzz Aldrin.
Obama amesema
Armstrong alikuwa shujaa wa kweli.
Picha za Armstrong akitembea mwezini zilionyeshwa moj kwa moja kwenye televisheni
Obama ameeleza kuwa wakati Armstrong na wanaanga wenzake walipoanza
safari yao katika chombo cha Apollo 11 mnamo mwaka wa 1969, waliyabeba
matumaini ya taifa lote la Marekani.
Wakati huo Obama alikuwa bado ana
wiki mbili ili kutimiza umri wa miaka minane.
Obama amesema, alipotembea
kwenye eneo la mwezini kwa mara ya kwanza ,Neil Amstrong alianzisha
kipindi cha mafanikio ya mwanadamu ambacho kamwe hakitasahaulika.
Mwanaanga mwenzake, aliefuatana naye katika safari ya mwezini,Buzz
Aldrin amesema ana uhakika kwamaba mamilioni ya watu wameungana naye
katika kuomboleza kifo cha shujaa huyo wa Marekani.
Buzz Aldrin amesema
atamkumbuka rafiki yake Armstrong kama jinsi wananchi wengine wa
Marekani na wote duniani watakavyomkumbuka mwanaanga huyo maarufu.
Licha ya mafanikio yake makubwa yaliyotokana na safari ya Apollo11
Armstrong hakuwa mpenda sifa wa vyombo vya habari na wakati wote
alijaribu kuviepuka.
Mondlandung 1969 Neil Armstrong Fußabdruck
Armstrong hakuhisi kujitoa hadharani na kuvitumia vyombo vya habari.
Hayo ameyasema mwanaanga mwengine wa Marekani John Glenn aliekuwa
Mmarekani wa kwanza kuizunguka sayari ya dunia. Wajerumani pia wametoa
rambi rambi zao juu ya kifo cha mwanaanga huyo wa Marekani na wamesifu
mafanikio yake.
Mkuu wa Shirika la utafiti wa anga la Ujerumani Profesa
Johann-Dietrich Wörner ameliambia shirika la habari la dpa, kwamba
Armstrong aliyawakilisha mafanikio ya maalfu ya wahandisi waliofanya
kazi kuifanikisha safari ya chombo cha Apollo 11.
Profesa huyo amesema Armstrong alikuwa ishara kwa binadamu ya
kuonyesha kwamba juhudi zao za kutafiti mambo mapya zitahifadhiwa daima
bila ya kujali iwapo utafiti huo utakuwa na faida kifedha.Profesa Wörner
amesema Arsmstrong ataacha urithi utakaokumbukwa daima duniani kote
hata baada ya kifo chake.
0 comments:
Post a Comment