Mahakama ya Norway yameamua kuwa Anders Behring Breivik ana akili zake
timamu, na imemhukumu kifungo cha miaka 21 kwa kuuwa watu 77 mwezi wa
Julai mwaka jana.
Upande wa mashtaka ukitaka kupata uamuzi juu ya akili ya Breivik, na
angekutikana punguani angewekwa kwenye jela ya wendawazimu kwa muda
usiojulikana.
Breivik siku zote amekiri kufanya mashambulio ya mabomu na bunduki, bila ya kuonesha majuto.
Amekuwa akishikilia kuwa ana akili yake, na kwamba aliyofanya ni vitendo vya kisiasa.
Alitabasamu hukumu ilipotolewa.
Wakili wa Breivik amethibitisha kuwa mteja wake hataomba rufaa.
0 comments:
Post a Comment