RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE.
MAKAZI YA MUDA YA WAKIMBIZI NDANI YA B ARA LA AFRIKA.
Ongezeko la wakimbzi katika mataifa mbali mbali ya bara la Afrika limepelekea serikali ya Kenya chini ya wizara ya sheria kuandaa mkutano wa siku mbili mjini Mombasa, kujadili changamoto zinazowakumba na namma ya kuimarisha ushirikiano baina ya wakimbizi na wenyeji.
Wajumbe kutoka mataifa ya Jumuiya ya Afrika mashariki na kati wanaoshiriki katika mkutano huo wamekubaliana kuhamasisha nchi zote husika ili kuanza kuondoa kasumba na unyanaypa na kutomtizama kila mkimbizi ni mhalifu au mwenye nia ya kufanya kitu kibaya ugenini.
Suala la ajira na rasilimali katika taifa linalowapokea wakimbizi limezungumziwa kuwa ni changamoto kuu hasa wenyeji wanapohisi kwamba wanatumia rasilimali zao pamoja na wageni.
Mfumo uliotumika na nchi ya Jamhuri ya kidemokrasi ya congo-DRC kuwapokea wakimbizi kutoka Rwanda na Burundi tangu mwaka 1971 umejadiliwa katika mkutano huu wa Mombasa.
Kenya ni moja wapo ya nchi inayowapatia hifadhi wakimbizi wengi, hasa kutoka Somalia, Ethiopia na Sudan Kusini, hata hivyo wale wanaopatikana wanaingia nchini humo kinyume cha sheria wamekuwa wakiishia gerezani au kurejeshwa katika nchi wanazotoka licha ya kuwepo machafuko ya kisiasa yanayoendelea huko.
Wakati huo huo Tanzania imetajwa kama mfano mzuri katika nchi za kanda ya maziwa makuu iliyoleta mabadiliko makubwa kwa wakimbizi kwa kuwapa uraia.
Huku Uganda ikisemekana kuweka sheria kali na kukosa kuwapa uraia wakimbizi walioishi katika taifa hilo kwa miaka mingi.
0 comments:
Post a Comment