Na Habiba Yahya, Morogoro.
HALMASHAURI ya wilaya ya Morogoro kwa kushirikiana na
idara ya afya inatarajia kuwafanyia upasuaji wa mabusha watu 80 wakati
wowote kuanzia sasa katika vituo vyake vya afya kwa lengo la kukabiliana na
tatizo hilo.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu msaidizi wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele wilayani humo Elias Lugata alisema kwa sasa dawa zimeshafika na kwamba taratibu za wataalam watahaohusika na kufanya upasuaji huo linaendelea.
Lugata alisema kuwa katika zoezi hilo halmashauri imetenga vituo vya afya vya Ngerengere,Mkono wa Mara,Dutumi na Tawa kwa lengo la kuwawezesha walengwa kufika kwenye vituo hivyo walivyo jirani navyo kupatiwa huduma hiyo.
Alisema fedha hizo zimetolewa na halmashauri kupitia mfuko wake(Basket fund) kwa lengo la kuwasaidia watu wenye tatizo hilo ili kudhibiti ongezeko na ugonjwa huo.
"unajua kuna watu wamekuwa wakifika kwenye vituo vyetu vya afya na kutaka kufanyiwa upasuaji kutokana na kutokuwa na uwezo wa kumudu ghrama za kufanyiwa upasuaji huo hivyo kutokana na hali hiyo halmashauri ikaona ni vyema ikatenga fedha kwa ajili ya kusaidia watu hao"alisema Lugata.
Alisema watu waliobainika ni wengi lakini tutaanza na watu hao na kwamba zoezi hilo litaendelea kulingana na uwezo utakavyoruhusu kwa lengo la kusaidia wananchi wa wilaya hiyo kukabiliana na tatizo hilo ambalo linakuwa kero kubwa kwa mhusika kutokana na kuharibu maumbile.
0 comments:
Post a Comment