Hali ya njaa nchini Mali.
MJUMBE maalum wa umoja wa mataifa wa haki za binadamu
Valerie Amos amesema kuwa dunia imeshindwa kuwajibikia hali ya hatari
kwa usalama wa raia wa Mali, ambako zaidi ya watu nusu milioni
wametoroka makwao kutokana na vita.
Bi Valerie Amos, ambaye amekuwa akizuru kambi za
wakimbizi ametoa wito wa msaada zaidi na ufadhili kuongezwa baada ya
jamii ya kimtaifa kukusanya tu nusu ya pesa zinazohitajika kukabiliana
na hali nchini humo.
Bi Amos yuko katika ziara ya siku tatu nchini Mali kujionea hali na athari za mzozo baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi.
Tangu hapo, wapiganaji wa kiisilamu wa kabila la Tuareg wameteka maeneo ya kaskazini mwa Mali.
Mwandishi wa BBC David Loyn, ambaye yuko katika
msafara wa Amos, anasema kuwa mzozo huo umeathiri pakubwa nchi hiyo na
kufanya rasilimali kuwa dunia kabisa.
Juhudi za kutoa msaada katika eneo la kaskazini zimeathirika kutokana na mapigano.
Bei ya juu ya vyakula pamoja na kipato cha chini zimesababisha hali ngumu kwa wananchi wa Mali.
Serikali mpya ya muungano, iliundwa katika mji
mkuu Bamako,mwishoni mwa wiki ikiahidi kuleta mageuzi na utahibiti
katika maeneo ya kaskazini mwa nchi.
Wapatanishi kutoka muungano wa nchi za magharibi
ECOWAS, wamefanya mazungumzo na wapiganaji hao, na hata kupeleka
wanajeshi elfu tatu nchini Mali ikiwa ni sehemu juhudi za amani
hazitazaa matunda.
Wapiganaji wa Tuareg waliteka eneo la kaskazini baada ya rais Amadou Toumani Toure kupinduliwa mwezi Machi.
0 comments:
Post a Comment