Maya Kodnani.
MAHAKAMA moja nchini India
imempata na hatia waziri wa serikali kwa kuhusika na mauaji ya halaiki
ya waisilamu tisini na tano wakati wa ghasia za kidini katika jimbo la
Gujarat miaka kumi iliyopita.
Maya Kodnani aliyekuwa waziri wa mambo ya
wanawake, alituhumiwa kwa kuchochea ghasia dhidi ya jamii za waisilamu
katika wilaya ya Naroda Patiya mjini Ahmedabad.
Alipatikana na hatia akiwa na mshtakiwa mwenzake
ambaye ni kiongozi wa wapiganaji wa kihindu Babu Bajrangi pamoja na
washukiwa wengine thelathini.
Ghasia za Gujarat zilizuka baada ya mahujaji sitini wa kihindu kufariki katika ajali ya Treni.
Zaidi ya watu elfu moja wengi wao wakiwa waisilamu waliuawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.
0 comments:
Post a Comment