BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAMASHA LA KUKUZA VIPAJI VYA WASANII WA MUZIKI, MAIGIZO NA KUCHEZA YAZINDULIWA MOROGORO.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Studio ya Town Record's Mohamed Ngwenje akizungumza jambo na wasanii vichupikizi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la wasanii la kuimba, kuigiza na kucheza likishirikiana na kituo cha Maendeleo ya vijana Tanzania lililoanza kwa vijana hao kushindana katika eneo la Lukobe Mgudeni Kihonda Manispaa ya Morogoro.

 Sar Green akirap kusaka moja ya nafasi 10 kwa upande wa rap katika tamasha hilo.
 Shedrack Paul akiimba kwa hisia katika tamasha hilo kwa nyimbo za taratibu.
 Denis Mwara akifokafoka katika mojawapo ya kuwania nafasi mojawapo ya ton ten kwa upande wa wasanii muziki katika siku ya kwanza ya tamasha hilo.
 Hapa mshikaji naye akivuta hisia wakati wa tamasha hilo la kuibua vipaji vya muziki, kuigiza na kucheza.
 Denis Mwara kushoto na Paul Lucas a.k.a Cash la Kanda kulia wakiwa katika pozi ya picha muda mfupi kabla ya kuanza kwa tamasha hilo.
Huyu mdada akionyesha namna ya kuigiza kabla ya kuanza kwa tamsha hilo huku akiwa na wenzake.

KITUO CHA UTAMADUNI NA MAENDELEO YA VIJANA TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA STUDIO YA MORO TOWN RECORD IMEZINDUA TAMASHA LA KUKUZA VIPAJI MKOANI MOROGORO.

KATKA TAMASHA HILO LINALOSHIRIKISHA VIJANA 250 KUTOKA MKOA WA MOROGORO NA PWANI IKIWEMO NA MAENEO YA KARIBU YALIANZA JANA MJINI KATIKA ENEO LA KIHONDA MJINI HAPA.

MKURUGENZI MTENDAJI WA STUDIO YA TOEN RECORD'S, MOROHAMED NGWENJE MOHAMED ALISEMA KUWA LENGO LA TAMASHA HILI NI KUIBUA VIPAJI VYA WASANII WACHANGA NA KUVIENDELEZA.

NGWENJE ALISEMA KUWA KWA UPANDE WA KUNDI LA WASANII WA MUZIKI WASHINDI 20 WAKIWEMO WAVULANA NA WASICHANA KILA KUNDI LITAPATA NAFASI YA KURECORD ALBAMU MOJA MOJA WAKATI WA MAIGIZO NAO WATAPATA FURSA YA KUTENGENEZEWA FILAMU MOJA YA MCHEZO WA MAIGIZO.

"WASHINDI WATAPATA BAHATI YA KURECORD ALBUM MOJA MOJA NA WASHINDI KWA UPANDE WA MAIGIZO WATAPATA BAHATI YA KUREKODI FILAMU" ALISEMA NGWENJE.

SHINDANO HILO  LITAKUWA LINARUSHWA MOJA KWA MOJA NA KITUO CHA LUNINGA CHA ABOOD YA MJINI MOROGORO ILI KUWAPA FURSA WATAZAMAJI YA KUWAPIGIA KURA WASHIRIKI WOTE KATIKA FANI ZAO.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: