Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete na familia
yake akijibu maswali toka kwa karani wa sensa ya watu na makazi, Clement Ngalaba wakati alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo lililofanyika kwa mafanikio makubwa nchi nzima ambalo limeanza jana.
TANZANIA imeanza zoezi la kuhesabu watu siku ya jumapili kwa muda wa siku saba.
Awali zoezi hilo lilionekana kuwa na upinzani mkali kutoka katika taarifa za kidini lakini taarifa zinasema zoezi limeanza bila matatizo yoyote.
Watu waliohesababiwa wameeleza kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa maafisa wa sensa ambao walizunguuka katika makazi mbalimbali ya watu kutekeleza zoezi hilo.
Jijini dar es salaam mwandishi wetu George Njogopa aliyefuatilia zoezi hilo kwa karibu anasema aliwaona maafisa wakipita nyumba mbalimbali ili kutekeleza zoezi hilo ambalo hufanyika takriban kila baada ya miaka mitano au kumi.
Kutoka na mfumo wa utaratibu huu, ikiwa kuna Mtanzani aliyoko nje ya nchi basi hatopata fursa ya kuhesababiwa.

0 comments:
Post a Comment