Amnesty International na Greenpeace wamezitaka Uingereza
kufungua kesi dhidi ya kampuni ya Kimataifa ya Trafigura kufuatia
kitendo chake cha kutupa taka za sumu nchini Cote d´Ivoire mwaka 2006
kwenye mji mkuu wa Abdjan.
Cote d'Ívoire inasema kuwa sumu hizo ambazo zililetwa na meli inayoitwa
Probo Koala chini ya usimamizi wa kampuni ya Trafigura zilisababisha
vifo vya watu 17 na kuwaathiri wengine maelfu kiafya.
Ripori ya mashirika hayo yenye kurasa 250 inasema na hapa nainukuu kuwa
" Serikali ya Uingereza ni lazima ianze uchunguzi wa kesi ya jinai kwa
kampuni ya Trafigura kwa kitendo chake hicho cha kutupa sumu hizo kwa
kuwa tawi la Kampuni hiyo la Uingereza ndilo lililoshirika kwa kaisi
kikubwa katika kuzua janga hilo.
Trafigura yakana
Meli ya Probo Koala iliyobeba takataka za sumu kuzipeleka Abdijan.
Hata hivyo kampuni ya Trafigura ambayo makao yake yako nchini Uswis
imekana kuwepo kwa uhusiano wowote baina ya sumu hizo na vifo vya watu
hao 17 pamoja na madhara mengine yanayotajwa kuwapata binadamu kutokana
nazo.
Katika tamko la kampuni hiyo, Tragura imeikosoa ripoti ya
mashirika hayo ikisema kuwa imerahisisha kupita kiasi masuala magumu ya
kisheria.
Mwezi Julai mwaka 2006, mabaki ya madini aina ya Caustic Soda na mafuta
ya petroli yakiwa yamepakiwa kwenye meli ya Probo Koala yalizuiwa
kuingia kupakuliwa ili yaweze kuchujwa kwenye bandari ya Amsterdam na
badala yake ylipelekwa mjini Abidjan ambako yalitupwa kwenye majalala ya
mji huo.
Taka hizo zikiwa zimewekwa kwenye matanki ya kusafishia petroli
inayotakiwa kusafishwa, yalirudishwa tena kwenye meli baada ya
kugundulika kuwa ni hatari zaidi kuliko ilivyodhaniwa mara ya mwanzo na
kampuni ya kuchuja sumu kwenye mabaki ya taka za kemikali ya Uholanzi
ilitaka kiasi kikubwa cha pesa kufanya kazi hiyo. Kampuni ya Trafigura
ilikataakulipa kiasi hicho cha fedha.
Amnesty International na Green Peace zinakikosoa kitendo hicho cha
kuyarudisha melini matangi hayo ya sumu yakisema kuwa ni uvunjifu wa
sheria za Uholanzi.
Katibu Mkuu wa Amnesty Salil Shetty anasema na hapa ninamkuu " Watu wa
Abidjan wa walidhuriwa si na serikali yao bali na serikali zote za Ulaya
ambazo hazikuhakikisha zinatumia sheria zao kuzuia kitendo kama hicho".
Mahakama nchini Uholanzi iliikuta kampuni ya Trafigura na makosa ya
kusafirisha sumu kutoka nchi hiyo kinyume na sheria, lakini waendesha
mashitaka hawakutilia maanani madhara yaliyoikumba Cote d´Ivoire baada
ya kutupwa sumu hizo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Green peace Kumi Naidoo anasema na
ninamnukuu " Bado hatujachelewa kwa sheria kuchukua mkondo wake, kwa
watu wa Abidjan kuelezwa hasa ni sumu gani zilitupwa na Trafigura
ikawajibika kutokana na makosa yake.
Kwa kufanya hivyo tu, ndio tunaweza
kuzuia makosa ya aina hii kufanywa tena hapo siku za baadae"
Ripoti hiyo imeonyesha mashaka juu ya sheria za Cote d´Ivoire ambazo
zinatoa mwanya kwa kampuni hiyo kukwepa mashataka yake kuendeshwa nchini
humo na hivyo imetoa wito kwa serikali kuhakikisha waatihirika wote wa
sumu hizo wanafidiwa kikamilifu.
0 comments:
Post a Comment