NA LILIAN LUCAS, MOROGORO.
CHAMA cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro MOPC Kimesitisha
kuandika habari za zozozte za polisi hadi pale baraza la habari MCT, Muungano
wa Clabu za waandishi wa habari UTPC na Jukwaa la wahariri watakapotoa
tamko rasmi juu ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha
televisheni cha Chanel 10 Daud Mwangosi yaliyosababishwa na polisi
wakati mwangosi akiwajibika kazini katika mkutano wa Chadema.
Mwenyekiti wa MOPC Aziz Msuya alisema hayo jana wakati
wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Morogoro wenye lengo la kutoa
tamko dhidi ya mauaji hayo.
Msuya alisema kuwa MOROPC inaungana na Clabu zingine za
waandishi wa habari nchini katika kulaani vikali mauaji hayo yasio na hatia kwa
mwandishi huyo na kwamba tukio kama hilo linaweza kumkumba mwandishi yeyote
hivyo inasatahili kulipinga nwa nguvu zote.
‘’ Mauaji hayo hayana msingi wowote kwa mwanataalumu huyo
ambaye alikuwa akiwajibika ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya habari
sasa kama waandishi wasipolipinga hilo litazidi kutokea kwa siku za usoni.
Alisema kuwa kwa kuwa vyombo hivyo ambavyo vinahusika
moja kwa moja na waandishi wa habari vinatarajia kutoa tamko juu ya kifo hicho
MOROPC imeamua kusitisha habari za polisi ili kusubiri tamko hilo.
Alisema kuwa ifahamike wazi kuwa
kazi ya polisi ni kulinda mali usalama wa watu na mali zao na sio kuuwa
kama walivyoamua sasa kujichukulia sheria mkononi.
Alisema kuwa hali hiyo inatishia na kudhoofisha utendaji
kazi wa waandishi wa habari na kuwafanya kuwa na woga na hivyo kuonyesha
dhairi kukiukwa kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini.
Kwa upande wake katibu wa chama hicho Abed Dogoli alisema
kuwa MOROPC imeandaa utaratibu wa kupeleka rambirambi kwa familia ya marehemu
huyo kama ilivyokuwa kawaida kwa wanataaluma hiyo kuungana pamoja wakati wa
shida na raha.
Aliwataka Familia ya marehemu kuwa na subira kwa kipindi
hiki cha majonzi ili kuweza kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo ambalo bado
linautata ndani yake.
0 comments:
Post a Comment