AJALI ya boti iliyotokea leo katika eneo la Ahmetbeyli nchini Uturuki
imesababisha vifo vya watu 58.
Boti hiyo ilikuwa imebeba wahajiri haramu
wasiopungua 100 na ilizama baada kugonga mwamba ilipokuwa ikikaribia
bandari ya magharibi ya Ahmetbeyli.
Wengi wa wahajiri hao walikuwa
kutoka nchi za Kiarabu. Baadhi ya manusura wamesema kuwa lengo lao
lilikuwa ni kufika Uturuki kisha kutumia njia za mkato kuingia barani
Ulaya.
Zaidi ya watu 40 wameokolewa kwenye ajali hiyo.
Makumi ya maelfu
ya wahajiri haramu hufa maji kila mwaka wakijaribu kuingia Ulaya kupitia
Uturuki na Libya na wengine hupoteza maisha baharini wakijaribu kuingia
Australia.
Baadhi ya nchi za Ulaya zimeweka sheria kali ili kukabiliana
na ongezeko la wahajiri haramu.
0 comments:
Post a Comment