CHAMA tawala nchini Angola cha MPLA chini ya rais Jose eduardo dos
Santos kimetangazwa rasmi kuwa kimeshinda uchaguzi wa bunge la nchi hiyo
uliofanyika Ijumaa iliyopita.
Vyombo vya habari vya serikali vilitangaza taarifa hiyo hata kabla ya
matokeo ya mwisho kutolewa.
Kwa hivyo, rais dos Santos anabakia miaka
mitano zaidi madarakani.
Wapiga kura wa Angola wakisubiri kushiriki uchaguzi mjini Luanda.
Kutokana na mabadiliko ya katiba ya mwaka 2010 ni kwamba kiongozi wa
chama kilichopata kura nyingi kabisa anakuwa rais na mkuu wa serikali.
Taarifa za Tume ya Uchaguzi iliyotangazwa katika mji mkuu wa Luanda
ilitaja kwamba asilimia 75 ya wapiga kura walikichagua chama cha MPLA.
Chama kikubwa kabisa cha upinzani, UNITA, kilipata asilimia 18 ya kura.
Msemaji wa upinzani na waangalizi huru wa uchaguzi hapo kabla
walilalamika kwamba kulikuweko kasoro katika zoezi la uchaguzi huo.
Jumla ya viti 220 vimeshindaniwa katika uchaguzi huo.
Uchaguzi umekwenda kwa amani.
Mamlaka nchini humo imesema kuwa zoezi la upigaji kura limefanyika kwa
amani.
Huu ni uchaguzi wa tatu nchini Angola tangu ipate uhuru wake
kutoka kwa Wareno mwaka 1975. Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 2008.
Kituo cha kupigia kura Angola.
Uchaguzi uliotangulia kabla ya huo wa mwaka 2008 ulifanyika mwaka
1992. Matokeo ya kutatanisha ya uchaguzi huo yalizusha awamu ya pili vya
vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hilo la kusini
mwa Afrika.
Katika uchaguzi wa safari hii, kwa mara ya kwanza Waangola walioko nje wanaoishi nchini Ureno wamekataliwa kupiaga kura.
José Eduardo dos Santos, Rais wa Angola.
Angola imepata mafanikio kiuchumi kutokana na mafuta. Hata hivyo
wachambuzi wameonya kuwa wakati wasomi wachache wananufaika, kundi kubwa
la raia wameendelea kubaki katika dimbwi la umasikini.
0 comments:
Post a Comment