Takriban wachimba migodi 50 wa
Afrika Kusini wameachiliwa huru na mahakama moja nchini humo baada ya
mahakama hiyo kutupilia mbali mashtaka yote dhidi yao.
Hatua hii inakuja siku moja baada ya wendesha mashtaka kufutilia mbali mashtaka dhidi ya wachimba migodi
270 kufutia shinikizo za uma.
270 kufutia shinikizo za uma.
Walifikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji ya wachimba migodi wenzao 34 waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Hapo awali polisi waliwapiga riasasi na kuwajeruhi wachimba migodi wanne katika tukio tofauti.
Inadaiwa kuwa polisi walitumia risasi za mipira
kuwatawanya waandamanaji katika Mgodi mwingine wa Gold Miners wanaogoma
wakidai nyongeza ya mishahara ndipo wanne hao walipojeruhiwa.
Kisa hiki kinafuatia kuuwawa kwa wachimba migodi wengine 34 wakati walipopigwa risasi na polisi wiki mbili zilizopita.
Mashtaka dhidi ya wachimba migodi waliofikishwa
mahakamani, kwa mujibu wa kanuni ya enzi ya ubaguzi wa rangi,
yaliakhirishwa kwa muda baada ya malalamiko ya umma.
Wachimba migodi wa kwanza miamoja walitarajiwa kuachiliwa leo wengine wakisubiri kuachiliwa siku ya Alhamisi.
Mazungumzo yanayolenga kusitisha mgomo wa
wachimba migodi hao wa mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana, vile
vile yalitarajiwa kuanza leo.
Polisi wanadai kuwa walilazimika kuwafyatulia
risasi wachimba migodi hao kama hatua ya kujilinda kwani na wao walikuwa
wamejihami kwa mapanga wakati wakikabiliana nao.
Mgomo wao ulioitishwa kulalamikia nyongeza ya
mishahara pamoja na kutaka chama chao kipya cha wafanyakazi kutambuliwa,
ungali unaendelea huku mgodi ukisalia kufungwa kwa wiki tatu sasa.
Hata hivyo kampuni inayomiliki mgodi huo,
Lonmin, ambayo ndio ya tatu kwa ukubwa wa uzalishaji wa madini hayo,
imesema kuwa mgomo huo ni haramu.
Lakini imetupilia mbali matakwa yake kuwa ikiwa wafanyakazi hao hawatarejea kazini , watafutwa kazi.
Baada ya ufyatuliaji risasi, viongozi wa
mashtaka wa serikali, walitumia kanuni ya enzi ya ubaguzi wa rangi ya
kosa la ujumla kuweza kuwafungulia mashtaka wachimba migodi 270
waliokamatwa wakati wa vurugu baada ya mgomo wao kuwalazimisha polisi
kuwafyatulia risasi.
Kanuni hiyo ilitumika na walowezi wa kizungu wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi kuwanyanyasa wapinzani wao waafrika weusi.
0 comments:
Post a Comment