NDEGE za kivita za jeshi la Kenya zimefanya mashambulio na kuvilenga vikosi vya jeshi la Somalia.
Kiongozi mmoja wa Somalia ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema
kuwa, tukio hilo lilitokea jana katika mji wa Ras Kamboni kusini mwa
nchi hiyo ambapo askari wapatao 51 wakiwemo wa Kenya na Somalia
wameuawa.
Amesema marubani wa ndege hizo walitekeleza shambulio hilo
pasina kufahamu kuwa eneo lililolengwa lilikuwa la vikosi vya serikali
ya Somalia likishirikiana na wanajeshi wa Kenya.
Somalia haina serikali madhubuti tangu mwaka 1991 juhudi za kurejesha
hali ya usalama na utulivu nchini humo zimekuwa zikigonga mwamba.
Vile vile watu wa kusini mwa nchi hiyo, mbali na kukabiliwa na vita, pia
wanasumbuliwa na ukame mkubwa.
0 comments:
Post a Comment