NDEGE za kijeshi zisizo na rubani za Marekani zimetekeleza shambulio
nchini Yemen na kuua watu wasiopungua 13.
Hayo yamethibitishwa na kingozi mmoja wa ngazi za juu wa Yemen ambaye
hakutaka jina lake litajwe na kuongeza kuwa, shambulio hilo
lililofanywa na ndege za Marekani zisizo na rubani, lilifanyika hapo
jana dhidi ya watu wanaodhaniwa kuwa na mahusiano na mtandao wa kigaidi
wa Al-Qaida.
Amesema kuwa, shambulio hilo halikuweza kupiga eneo husika
na badala yake lililenga magari mawili ya raia katika mji wa Radda
unaopatikana katika mkoa wa Al Bayda ambapo watu 13 waliuawa papo hapo
wakiwemo wanawake wawili na wengine wakijeruhiwa vibaya.
Wananchi wa Yemen wamekuwa wakipinga vikali uingiliaji wa Marekani nchi
mwao sambamba na kufanya maandamano makubwa huku wakitoa nara za "Mauti
kwa Marekani, Mauti kwa Israel."
Mbali na Wayemeni hao kupinga uingiliaji wa Marekani nchini kwao,
wanapinga na kulaani mashambulizi ya ndege hizo zisizo na Rubani nchini
humo ambayo mwezi uliopita yaliua idadi kubwa ya raia wasio na hatia.
Hivi karibuni Rais Barack Obama wa Marekani alijigamba akidai kuwa, kila
Mmarekani anaona fakhari kwamba nchini yake ina nguvu na inaheshimiwa
kwa kuendesha vitani zaidi duniani.
0 comments:
Post a Comment