MAKUMI ya wafungwa wameripotiwa kutoroka jela nchini nchini Ivory Coast.
Vyombo vya mahakama za nchi hiyo vimeripoti kuwa wafungwa 25 wa jela katika mji wa Daloa walitoboa tundu katika ukuta wa jela hiyo na kufanikiwa
kutoroka.
Askari usalama wa nchi hiyo wamefanikiwa kuwakamata watano
miongoni mwao na wengine hawajulikani waliko.
Mkurugenzi wa Mashtaka wa mji wa Daloa ameamuru kufanyike uchunguzi kuhusu tukio hilo na kuchukuliwa hatua kwa maafisa waliozembea.
Vituo vya serikali, jeshi na polisi ya serikali ya Ivory Coast
vimekuwa vikishambuliwa na makundi yenye silaha katika siku za hivi
karibuni na inadhaniwa kuwa wafuasi wa rais wa zamani wa nchi hiyo
Laurent Gbagbo ndio wanaohusika na mashambulizi hayo.
0 comments:
Post a Comment