SOUTHAMPTON katika mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya England leo jumapili ambapo katika mchezao huo Man United ilishinda kwa bao 3-2 kupitia kwa mshambuliaji huyo.
Mshambuliaji mpya wa Arsenal
TIMU ya Liverpool ya Uingereza imekubali kipigo cha mabao 2-0 mbele ya
Arsenal katika uwanja wake wa nyumbani.
Liverpool leo jioni (Jumapili) walikuwa wenyeji wa Gunners (Arsenal)
katika wiki ya tatu ya ligi ya Premier ya Uingereza na imeshindwa
kuhimili mikiki ya vijana wa mkufunzi Arsene Wenger.
Walikuwa ni vijana wapya wa Arsenal, Lukas Podolski na Santi Cazorla
ndio ambao waligawana fursa za kutoa kipigo hicho kwa Liverpool kila
mmoja kwa wakati wake katika vipindi viwili vya pambano hilo.
Alikuwa ni Lukas Podolski aliyeanza kuliona lango la Liverpool katika
dakika ya 31 lililodumu hadi mwishoni mwa dakika 45 za kipindi cha
kwanza.
Dakika ya 68 ya mchezo huo ilikuwa ni wakati wa Santi Cazorla
kudidimiza msumari wa mwisho kwenye jeneza la Liverpool leo hii.
Kwa ushindi huo Arsenal imepanda hadi nafasi ya 7 ya msimamo wa ligi
hiyo ya Premier kwa kuwa na pointi 5 baada ya kucheza mechi tatu.
Chelsea ndiyo inayoongozwa msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 9 na
imecheza meshi tatu.
Baada ya kuchezea kipigo cha leo, timu ya Liverpool imeporomoka hadi
kwenye nafasi ya 17 ya msimamo wa ligi hiyo.
MATOKEO YA LEO KATIKA LIGI HIYO YAMEKUWA HIVI:
Newcastle 1-1Aston Villa
Liverpool 0-2 Arsenal
Southampton 2-3 Man Utd
- MATOKEO YA JANA:
- West Ham 3-0 Fulham
- Swansea 2-2 Sunderland
- Tottenham 1-1 Norwich
- West Brom 2-0 Everton
- Wigan 2-2 Stoke
- Man City 3-1QPR.
0 comments:
Post a Comment