HIVI NDIVYO ILIYOKUWA KATIKA MJI WA MUFINDI KATI YA POLISI NA CHADEMA NA KUDAIWA MWANDISHI CHANEL TEN KUFARIKI DUNIA. PICHA hii ndiyo ikionyesha namna mwandishi wa habari wa Chanel Ten Daud Mwangosi akiwa chini sehemu ambayo inadaiwa kufariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa na askari wa jeshi la Polisi mkoani Iringa mkoani jana.Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi.
Mwili unaodaiwa kuwa ni mwanahabari wa habari kituo cha chanel ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi ukiwa chini kabla ya kuondolewa.
ENZI ZA UHAI WAKE DAUD MWANGOSI. MWANDISHI wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi anadaiwa kufariki dunia wakati wa vurugu baina ya askari wa jeshi la polisi i na wafuasi wa chama cha maendeleo na demokrasin (Chadema) katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Mwandishi aliyetambuliwa kwa jina la, Daud Mwangosi anadaiwa kufariki dunia majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi.
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kwa madai kuwa hapo walipo ndipo katika ofisi zao.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa, Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadaye inadaiwa mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari
JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.
Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.
" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza
Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.
"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.
Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.
Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .
Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.
"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa.
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .
Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.
"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa.
sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao
watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano
yetu ?.
tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida
hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.
Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .
Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .
habari kutoka vyanzo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment