BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DKT LARAJINI: ISRAEL TISHIO KWA ULIMWENGU WA KIISLAM

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/4caea1c6322ef6c34a21f9f277ec35c7_L.jpg 

DKT LARIJANI.

DAKTARI Ali Larijani mabye ni Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ni tishio kubwa kwa usalama na uthabiti wa ulimwengu wa Kiislamu. 

Dakta Larijani alisema kuwa mataifa ya Kiislamu yanapaswa kufanya hima kubwa kwa ajili ya kuzikomboa kikamilifu ardhi za Palestina na kuhakikisha kwamba wananchi hao madhulumu wanarejeshewa haki zao zilizoghusubiwa na Wazayuni. 

Spika wa Bunge la Iran alisema hayo wakati mazungumzo na Hassan bin Talal mjumbe maalumu wa Mfalme wa Jordan aliyeyopo nchini Tehran kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote dunani NAM. 

Larijani ameashiria changamoto muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu na kubainisha kwamba mataifa ya Kiislamu yanaweza kukabiliana na changamoto hizo pamoja na njama za madola ya kibeberu kwa kudumisha umoja na mshikamano baina yao.  

 CHANZO:kiswahili.irib.ir

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: