Mchezaji wa timu ya Ras Mtwara Sport Club, Mpesa kulia na Flora Mandikisi kushoto wakijaribu kumzuia mchezaji wa Viwanda Regina Kavenuke (katikati) bila mafanikio wakati wa mchezo wa netiboli baina ya timu hizo katika mashindano yanyoendelea ya shirikisho la Michezo ya Idara za Serikali, Wizara na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo katika mchezo huo Viwanda walikuba kufungwa kwa vikapu 30-17.
Mchezaji
wa timu ya Ras Mtwara Sport Club, Lucy Kachenga mbele akijaribu kudaka
mpira huku akizongwa na mchezaji wa Viwanda Faith Thawe katika mchezo huo.
TIMU ya Ras Mtwara Sport Club imejigamba kufanya vizuri katika mchezo wa netiboli huku ikiweka mikakati kabambe ya kuvuka hatua ya makundi kufuatia kuanza vema mbio za kutwaa ubingwa huo kwa kupata ushindi mnono dhidi ya timu ya Viwanda katika mashindano yanayoendelea ya shirikisho la Michezo ya Idara za Serikali, Wizara na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) yanayofanyika katika viwanja vya Ulinzi na Jamhuri mkoani Morogoro.
Wakizungumza na gazeti hili katika uwanja wa Jamhuri viongozi wa timu ya Ras Mtwara walisema wanashurku kwa kuanza vema mashindano hayo na kupata ushindi mnono dhidi ya Viwanda wa vikapu 30-17 ambapo ni tegemeo kubwa ambalo wameelekeza kwa kurudi na kombe ni katika mchezo wa netiboli licha ya kuwa na michezo mingine inayoshiriki mashindano ya Shimiwi kwa mwaka 2012.
Kocha mkuu wa mchezo wa netiboli, Devotha Koka alisema kuwa kwa upande wa mchezo wa netiboli wana uhakika wa kuvuka hatua ya makundi na kuingia katika hatua ya robo fainali kisha kufika nusu fainali kutokana na uimara wa kikosi chao baada ya kupata maandalizi ya kutosha kwenye mashindano hayo.
Koka alisema kuwa wamefurahi kupata ushindi katika mchezo wa kwanza kwani vijana wake wametekeleza maagizo yake na kuifanya timu yao kuanza vizuri harakati za mbio za kugombea ubingwa wa kombe hilo na kuwa wameelekeza kufanya mazoezi ya nguvu ili kuweza kushinda tena mchezo wa pili dhidi ya Utumishi utaofanyika Septemba 26 ambapo wataongeza kasi ili kuweza kuishinda timu hiyo na kujiweka katika mazingira mazuri ya kupata nafasi ya kwanza na kusonga mbele.
Naye Katibu wa Ras Mtwara Sport Club, Mussa Chimae alisema kuwa mashindano ya Shimiwi 2012 Ras Mtwara imeshirikisha jumla ya timu tano ikiwemo netiboli, riadha, bao, draft na karataya na kuwa tegemeo pekee ya kurudi na kombe lipo katika mchezo wa netiboli ambapo wameelekeza nguvu zaidi katika mashindano hayo.
Chimae alisema kuwa si netiboli tu ambayo imepewa nguvu kubwa lakini pia kuna michezo mingine ya ndani nayo imepewa imeweke mikakati ya kuishinda na kudai kuwa suala ya kuipa kipaumbele mchezo wa netiboli umetokana na kupata maandalizi ya kutosha tofauti na michezo mingine.
Katika mashindano hayo ambayo yamenza kutimua vumbi Septemba 22 ilishuhudia timu ya Ikulu ikiibuka na ushindi wa 41 dhidi ya Elimu katika mchezo wa ufunguzi netiboli huku katika upande wa soka Hazina ikikubali kipigo cha cha bao 1-0 kutoka kwa Ukaguzi katika michezo iliyochezwa uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Lakini timu hiyo imejikuta ikiaga mashindano hayo baada ya kupoteza michezo mitatu na kushinda kuvuka hatua ya makundi ambayo inamalizika kesho Septemba 29/09/2012.
0 comments:
Post a Comment