WATU saba wamepoteza maisha baada
ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya madini yaliyopo katika kata ya Nandagala
wilayani ya Ruangwa mkoani Lindi.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hii Diwani wa kata hiyo, Andrew
Chikongwe alisema kuwa kazi ya kufukua kifusi na kutoa miili ya marehemu
hayo ilianza majira ya saa 9 alasiri hadi mapema asubuhi huku wakifanikiwa
kupata miili yote.
Chikongwe alisema kuwa kazi hiyo
ilikuwa ngumu kutokana na kuwepo kwa zana duni za uokoaji wakati wa kufukua mchanga
na hatimaye kupata miili hiyo.
Diwani huyo aliwataja marehemu hao
kuwa ni Nyang'ana Mkelecha mkazi wa Musoma, Mohamed Omari Fondogoro Mkazi
wa Morogoro, Bakari Liganga mkazi wa Chunyu Ruangwa.
Wengine ni Rajab maarufu ROGER mkazi
wa Musoma, Uwesu Bakari Abeid mkazi wa Rondo ,Chakoda mkazi wa Dar na
Rashid Ally maarufu BADE mkazi wa Masasi mkoani Mtwara.
0 comments:
Post a Comment