Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora
wa sera ya Kilimo na Chakula toka kwa Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya
kiserikali inayohusika na sera za kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo kama Food,
Agriculture
and Natural Resources Policy (FANRPAN)
katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012. Anayeshuhudia kulia
ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo
hutolewa kwa kiongozi
aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora za kilimo na chakula
nchini kwake,
ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana,
wakati Rais
Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza
mwaka
2009 na Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa
Mutharika, aliipokea mwaka 2008.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akiangalia baadhi ya ng'ombe anaowafuga kwa kufuata njia za
kisasa kwenye shamba lake kijijini kwake Msoga, Chalinze, Wilaya ya
Bagamoyo, leo Septemba 6, 2012.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment