WAKUU wa nchini ya Guinea wanasema kuwa watu kama 30 wamekufa kwenye ajali ya mashua katika bahari ya Atlantic.
Inaarifiwa kuwa mashua hiyo ilikwenda mrama kwa
sababu ya dhoruba wakati ikisafiri kutoka mji mkuu, Conakry, kuelekea
kisiwa cha Kassa, safari ya kilomita 10.
Shughuli za uokozi zimesimamishwa.
Ajali kama hizo zinatokea mara kwa mara nchini
Guinea na kwengineko Afrika, ambako mashua hupakia abiria wengi na
hazitazamwi sawa sawa.
0 comments:
Post a Comment